Mwanaharakati na Mtetezi wa haki za binadamu Tito Magoti amefungua kesi ya kikatiba mahakama Kuu kuiomba mahakama hiyo ifute sheria inayozuia wafungwa kupiga kura.Wanaoshitakiwa ni Tume ya Uchaguzi,Mwanasheria mkuu wa serikali,Tume ya haki za Binadamu na Watu na Magereza.
Pia katika shauri hilo namba 3/2022 anaiomba mahakama itoe tamko la kutotimiza wajibu na amri ya kulipwa fidia kwani kutokana na uzembe wa washitakiwa yeye (Tito) pamoja na wafungwa wengine hawakuwekewa mazingira ya kupiga kura mwaka 2020 ingawa hakuna sheria iliyowazuia hivyo wanaiomba mahakama ilinde haki ya wafungwa na mahabusu kushiriki uchaguzi hasa kupiga kura.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 7 Machi mwaka huu mbele ya Jaji Mgeta na wapeleka maombi watawakilishwa na Wakili John Seka.
Tito Magoti ambaye ni Afisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) aliwahi kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi mnamo mwaka 2019,yeye pamoja na mwenzake Theodory Giyani walikaa gerezani kwa takribani mwaka mmoja na wakati uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unafanyika alikuwa gerezani
Wawili hao walisomewa mashitaka ya kuongoza genge la uhalifu,kumiliki program ya kompyuta iliyotengenezwa kwa lengo la kufanya uhalifu na kutakatisha fedha kiasi cha Milioni 17,makosa ambayo hayana dhamana, kesi hiyo iliendeshwa kwa muda wote bila kusikilizwa kwani upende wa serikali ulidai kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo haujakamilika.
Magoti na mwenzake waliachiwa huru kupitia mfumo wa kukiri na kukubali makosa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na kuamriwa kulipa faini ya Milioni 17 pia mahakama ya hakimu mkazi kisutu ilitoa hukumu kwa wawili hao kutokutenda makosa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA