March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Shirika la C-SEMA wameendesha mafunzo kwa maofisa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na Mawakili kutoka ofisi ya Taifa ya mashtaka.
Mafunzo hayo yamefayika kwa siku mbili ambapo yalianza Agosti 17, 2022 katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha washiriki kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.
Akizugumzia juu ya mafunzo hayo Mratibu wa Mtandao huo Kitaifa, Onesmo Olengurumwa alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kukumbushana kuhusu misingi ya haki za binadamu na kujadili changamoto zilizopo hususani masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na unyanyasaji wa watoto ili kushauriana namna bora ya kuzitatua.
Mafunzo hayo yamezinduliwa na Mgeni rasmi, Kamishina wa Kamisheni ya Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, (IGP) Camilius Wambura.
(CP), Fausitine Shilogile alisema kuwa licha ya jitiada zinazoendelea kufanyika lakini matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto yamekuwa yakiendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali Nchini, Hivyo aliwaelekeza Maofsa Upelelezi wa Polisi Mikoa (RCO) kutoacha matukio ya ukatili wa kijinsia kushughulikiwa tu na maofisa wa madawati ya Ukatili wa kijinsia.
Aidha mafunzo hayo yaliongozwa na wachokoza mada akiwemo Mh. Jaji mstaafu Robert Makalamba, Mkuu wa kitengo cha Utetezi THRDC, Wakili Leopold Mosha, Afsa Uchechemuzi THRDC, Nuru Maro na maofisa wengine kutoka kwenye mamlaka zilizoshiki mafunzo hayo.
Katika Mafunzo hayo wameweza kuzungumzia zaidi kuhusu masuala ukatili wa kijinsia pamoja na unayanyasaji wa watoto ambapo washiriki wengi wameweza kushiriki kuchangia maoni pamoja na kutoa mifano ya matukio yanayohusu maeneo hayo kwa lengo la kupeana uzoefu.
Mafunzo hayo yamefungwa na Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, (DCI) Ramadhani ingai ambaye amewataka maofisa wa upelelezi kwenye Mikoa kufuatilia kwa ukaribu kesi za ukatili wa kijinsia pamoja na unayanyasaji wa watoto, lakini amesisitiza wazazi kuzingatia suala la malezi bora kwa watoto wao hususani watoto wa kike jambo ambalo amedai kuwa linaweza kupunguza matukio ya ukatili.
Itakumbukwa Julai 25, na 26, 2022 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Kanda ya Pwani ya Kusini na Shirika la Door of Hope waliendesha mafunzo ya aina hiyo kwa maosifa kutoka Mikoa ya Kusini katika Hoteli ya Tiffany Diamonds mkoani Mtwara.
Hata hivyo Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa kadili watavyokuwa wanafanikiwa kupata uwezo wa kifedha wataendelea na mafunzo hayo kwenye Kanda zingine ikiwemo na Zanzibar pia kupanua wigo wa washiriki kutoka mamlaka muhimu ambazo zinashughukia masuala yaliyowakutanisha, ambapo ametolea mfano juu ya kuwajumuhisha maafisa kutoka kwenye madawati ya kijinsia na watoto pamoja na mahakimu ikiwa lengo ni kuhakikisha hiki zinastawi kila eneo Nchini.