
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la American Bar Association (ABA),linaendesha mdahalo kuhusu kesi za Maslahi kwa Umma,(Public Interest litigation).Mdahalo huo uliofunguliwa na Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo,Wakili Onesmo Olengurumwa umehudhuriwa na Muwakilisha wa Shirika la ABA ukanda wa Afrika Mashariki,Bi. Violah Ajok na unashirikisha wanafunzi zaidi ya 200 wanaosoma katika shule kuu ya Sheria Tanzania,mawakili,wandishi wa Habari,na wadau wengine wa masuala ya sheria na haki za binadamu kutoka nje ya Tanzana wanaoshiriki kwa njia ya Mtandao (Zoom).
Wazungumzaji wakuu katika Mdahalo huo unaofanyika katika ukumbi wa Bomani,Shule Kuu ya Sheria Tanzania,ni pamoja na nguli wa Sheria nchini Tanzania,Profesa Issa Shivji,na Jaji Mkuu Mstaafu,Profesa Robert Makaramba.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.