March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC- ZANZIBAR WAINGIA MAKUBALIANO NA MAHAKAMA, WAWEKA MIPANGO KABAMBE, KUGUSA MAENEO SUGU YA HAKI

Na: Anthony Rwekaza

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kupitia tawi lake la Zanzibar (THRDC-Zanzibar), Ijumaa Januari 14, 2022 umesaini hati ya makubaliano (MOU) kati yake na Mahakama ya Zanzibar kwa lengo la kukuza na kuboresha mfumo wa utoaji haki na kukuza Haki za Binadamu Visiwani Zanzibar.

Akizungumzia tukio Mratibu wa THRDC Zanzibar, Abdallah Abeid amesema hatua hiyo imekuja baada ya kazi nzuri wanayoifanya, ameeleza kuwa kwa kuanza kwa kushirikiana na Mahakama kwamba kunazaa matunda hvyo wameona umuhimu wa kurasimisha ushirikiano huo, lakini pia amesisitiza kwamba mahusiano hayo yatakwenda kujenga mfumo imara zaidi wa utoaji haki ambao …
[11:06 AM, 1/15/2022] Antony CV Volu Watetezi TV: THRDC- ZANZIBAR WAINGIA MAKUBALIANO NA MAHAKAMA, WAWEKA MIPANGO KABAMBE, KUGUSA MAENEO SUGU YA HAKI

Na: Anthony Rwekaza

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kupitia tawi lake la Zanzibar (THRDC-Zanzibar), Ijumaa Januari 14, 2022 umesaini hati ya makubaliano (MOU) kati yake na Mahakama ya Zanzibar kwa lengo la kukuza na kuboresha mfumo wa utoaji haki na kukuza Haki za Binadamu Visiwani Zanzibar.

Akizungumzia tukio Mratibu wa THRDC Zanzibar, Abdallah Abeid amesema hatua hiyo imekuja baada ya kazi nzuri wanayoifanya, ameeleza kuwa kwa kuanza kwa kushirikiana na Mahakama kwamba kunazaa matunda hvyo wameona umuhimu wa kurasimisha ushirikiano huo, lakini pia amesisitiza kwamba mahusiano hayo yatakwenda kujenga mfumo imara zaidi wa utoaji haki ambao Wananchi watakuwa wanufaika wa moja kwa moja.

Pia Mratibu huyo ambaye anashughulika na upande wa Zanzibar, ameongeza kuwa THRDC imejitoa kushirikiana na Mahakama ili kuhakikisha kwa pamoja wanaimarisha mfumo wa utoaji haki visiwani Zanzibar. Ameweka wazi kuwa wanaamini kuwa mashirikiano hayo yatazaa matunda ambayo yatapelekea kujivunia makubaliano walioingia ya miaka mitatu, lakini pia ameishukuru Mahakama kwa kujenga imani ya kushirikiana.

“THRDC tumejitoa moja kwa moja kushirikiana na Mahakama kuhakikisha mfumo wa utoaji haki unaimarika na kufanya kazi vizuri visiwani Zanzibar, ni imani yetu kwamba mashirikiano haya yatazaa matunda na tunajivunia makubaliano haya ya miaka mitatu. Tunaishukuru Mahakama kwa kujenga imani ya kushirikiana na sisi kufanya kazi na kuhakikisha tunaimarisha mifumo ya utoaji haki hapa Zanzibar” amesema Mratibu THRDC- Zanzibar, Abdallah Abeid

Aidha Mratibu THRDC Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kwa muda mfupi ambao THRDC imesajiliwa visiwani Zanzibar wamefanya za ushirika na taasisi nyingi za Serikali, lakini ameongeza kuwa wanategemea kufanya mambo mengine zaidi wakiwa na malengo ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Zanzibar hususani kukuza usawa na haki.

“Kwa muda mfupi tangu kusajiliwa kwa tawi la THRDC visiwani Zanzibar, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu umefanya kazi za ushirika na tasisi nyingi za serikali na wanategemea kufanya mengi kwa malengo ya kuwaletea maendeleo wazanzibari ikiwamo kukuza usawa na haki za binadamu” amesema Mratibu Kitaifa – THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Vilevile kwa upande wa Mahakama visiwani, kupitia Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdallah amedai kuwa Mahakama imekuwa na matatizo mengi hivyo wamedhamiria kufanya maboresho ya kiutendaji, ambapo amesema kuwa wamedhamiria kuyaondoa matatizo hayo ili kuwafanya wananchi kunufaika na huduma zinazotolewa na Mahakama na kupunguza malalamiko.

“Mahakama imedhamiria kufanya maboresho ya utendaji wake. Kama nilivyoeleza mahakama imekumbwa na matatizo mengi, kwa hiyo tumedhamiria kuyaondoa kabisa hayo matatizo ili wananchi wapate kufaidika na huduma zinazotolewa na mahakama na kupunguza malalamiko” amesema Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdallah

Lakini katika kuonesha umuhimu wa wadau kama THRDC katika masuala yanayofungamana na haki, Jaji Khamis Ramadhani amesema Mahakama haiwezi kutekeleza majukumu yake peke yake licha ya kuwa chini ya Serikali amedai kuwa kuna wadau wengine ambao Mahakama inashirikiana nao ili kufanikisha lengo lao la kufanya maboresho, ameweka wazi kuwa kati ya wadau hao ni ambao tayari wamejitokeza ni Mtandao wa Watetezi wa Haki Binadamu Tanzania (THRDC), ambao amesema kuwa kupitia tawi lao jipya la Zanzibar wameanza kushirikiana nao.

“Mahakama haiwezi kutembea peke yake, tupo chini ya serikali lakini kuna wadau wengine ambao tunashirikiana nao kuhakikisha tunafikia lengo letu la kufanya maboresho, mojawapo ya wadau waliojitokeza ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ambao kupitia tawi lake la Zanzibar wamekuja na kuanza kushirikiana nasi” amesema, Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdallah

Kwenye makubaliano ambayo wamekubaliana kuwa na mashirikiano katika utekelezaji ni kwenye maeneo manne ambayo ni, kujenga uwezo wa kutoa haki katika jamii, mfano kufanya tafiti na kutengeneza ‘document’ itakayoainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama na namna ya kuzitatua.

Pili, Ufanyaji tafiti katika maeneo mbalimbali ikiwemo maswala ya udhalilishaji wa kijinsia.
katika eneo hilo Kaimu Jaji Mkuu, amesema wanaweza kufanya tafiti za sababu zinazopekea ukatili wa kijinsia na nmna ya kuzikabili, amesema tatizo hilo limekuwepo katika jamii.

Eneo la tatu ambalo ambalo wakubaliana ni, Usimamizi wa mashauri (case management). Kaimu Jaji Mkuu katika eneo ili ameweka wazi kuwa wanajua uwepo wa tatizo la usimamizi wa mashauri, na kuwa yapo malalamiko kwamba mashauri hayaendi kwa haraka, hukumu hazitoki kwa haraka, ‘proceedings’ hazitoki kwa haraka, hivyo kufuatia madai hayo amesema katika mashirikiano yao watatafuta namna nzuri na ya kisasa ya kusimamia mashauri.

Eneo la nne ambalo lijumuhishwa kwenye mashirikiano hayo ni, kushirikiana katika kuendesha semina na ‘refresher Courses’ kwa lengo la kuboresha huduma za kimahakama.

Ikumbukwe THRDC ambayo imekuwa ikitekeleza majukumu yake yanayogusa haki za Binadamu hivi karibuni imepanua wigo wa Haki kwa kufungua tawi jipya visiwani Zanzibar ambalo inaelezwa kuwa litakuwa likitekeleza majukumu visiwani humo kama tayari ambavyo limeanza, itakumbukuwa hata upande wa Zanzibar kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazogusa Haki za Binadamu licha ya Serikali kwa mara tofauti kupitia viongozi mbalimbali kugusia, kupinga na kuwekea msisitizo juu ya masuala yanayoweza kuwa chanzo cha kuvuja Haki za Binadamu.