Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TRA imekutana na wadau wa Asasi za Kiraia katika semina wezeshi juu ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Asasi za kiraia ni moja kati ya maeneo yanayochangia kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato kutokana na kupokea fedha za miradi mbalimbali,utekelezaji miradi,pamoja na ajira.
“THRDC kwa kushirikiana na Asasi zingine kama ACT2,Wajibu Institute na mashirika yote kupitia Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia tumeona umuhimu sana wa muda mrefu wa kuwa karibu na mamlaka ya mapato Tanzania ili kupata uelewa wa taratibu na sheria ambazo zinahusu masuala ya kodi na sisi tutakuwa tumepata faida ya kuweza kufuata zile taratibu tunazotakiwa kufuata kama Azaki,” amesema Wakili Onesmo Olengurumwa,Mratibu Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (THRDC).

Aidha mtandao huo umeiomba mamlaka ya Mapato kufikiria zaidi namna bora ya utozaji wa kodi utakaowezesha wanachama wengi zaidi kulipa kodi bila shuruti.
“Asasi za kiraia hazina fedha zake ni fedha za wahisani,kama kuna madeni yaweze kuombewa msamaha riba na kodi ili waweze kulipa kwasababu ukiangalia zinalipika zingine.Kama mamlaka yako (TRA) inaweza ikaongea na mamlaka zingine angalau AZAKI kwa zile zilizokuwa zinadaiwa zikapewa muda fulani wa kulipa malimbikizo kama yapo bila kuwa na riba na pelnati ili kuwaruhusu kuanzia sasa kwavile tumetoa mafunzo kusiwe na mazingira kama hayo kuweza kujitokeza,”ameongeza Olengurumwa katika semina hiyo ambayo pia mwongozo wa uwajibikaji wa Sheria zinazoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya wanachama wa mtandao huo.

Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa licha ya Asasi za Kiraia kuchangia kwa kiasi kikubwa ulipaji kodi, bado serikali imekuwa haitambui bayana mchango huo na hivyo THRDC imeishauri serikali kupitia mamlaka hiyo kutambua mchango wa azaki katika taarifa zake za kikodi ili kuleta hamasa kwa wadau wa sekta hiyo kuwa marafiki wa kodi.
Mamlaka hiyo imepongeza hatua ya THRDC kuona umuhimu wa kuitakutanisha na wadau wa Azaki na kuyataka pia makundi mengine yenye umoja kufanya hivyo ili kuleta uelewa wa pamoja wa masuala ya kodi.Vilevile Mamlaka hiyo imekiri kuwa sekta ya Azaki imekuwa mbia mkubwa wa ulipaji kodi.
“Kwa kipindi cha miaka miwili,sekta ya azaki imekuwa na mchango mzuri sana katika suala la ulipaji kodi tangu tulipokaa nanyi kule Mwanza mwaka 2019”,amesema Richard Kayombo,kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuongeza kuwa Azaki ni moja kati sekta tatu zinazochochea maendeleo.
Semina hiyo inayojumuisha wana Azaki zaidi ya 150 inafanyika siku moja kabla ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kuadhimisha kwa mara ya 7 siku ya Watetezi wa haki za binadamu maarufu kama “Defenders Day” inayotarajiwa kufanyikaJulai 2 jijini Dar es Salaam baada ya kushindikana kufanyika mwaka 2020 kwa sababu zilizokuwa nje ya mtandao huo.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.