December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC YAWAKUTANISHA MAWAKILI WA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR.

Baadhi ya washiriki wanaoshiriki Mafunzo,Unguja.

JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman, amesisitiza kuwa,kuheshimu haki za Binadamu ni jambo muhimu kwa sababu ni stahili yay a kila mtu anayopaswa kupewa ,Kauli hiyo ametoa kama mgeni rasmi katika hotuba yake aliyowasilisha wakati  wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa mawakili na wanasheria Zanzibar wanaojishughulisha na utetezi wa haki za Binadamu,iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania,THRDC chini ya Ufadhili wa taasisi ya Kimataifa ya American Bar Association,(ABA).    

Jaji Othman shauku ya kuwaona mawakili  wanaohudhuria mafunzo hayo wanakuwa mabalozi wazuri  wa kulinda na kutetea haki za binadamu katika ubora wa kiwango kinachokubalika Kimataifa.

Omar Othman Makungu-Jaji Mkuu wa Zanzibar.

“Masuala ya Haki za Binadamu ni katika vitu vya msingi sana,ni stahiki ya kila binadamu”-amesema jaji huyo na kuongeza kuwa masuala ya haki za Binaadamu ni kati ya vitu vya msingi na kwamba kuwanyima watu haki zao, ni kukosa ubinadamu kwa kiwango cha juu no.

Jaji mkuu huyo amesema matumaini i yake mkusanyiko huu pamoja na mambo mengine utajadili namna ambavyo mawakili wanapaswa kuendesha kesi zenye maslaqhi kwa umma, haki za binaadamu, uhuru wa kujieleza kwa viwango vya kitaifa na vile vya kimataifa.

Katika mafunzo hayo  ya siku mbili,washiriki (mawakili) watajifunza  pia ufunguzi wa mashauri ya kimkakati na mambo mengine yenye mnasaba na utekelezaji wa haki za binadamu na amewaomba washiriki hao kuwa makini maana  masuala yaliyopangwa kujadiliwa yanawagusa watu moja kwa moja katika maisha ya kila siku.nagusa msingi na heshima ya ubinaadamu.

“ Haki za Binadamu ni kati ya vitu vya msingi sana kwa vile yanagusia stahiki ambazo zinampaswa kila binaadamu kuzifaidi kwa kuwa yeye ni binaadamu. Haki hizi kwa lugha nyengine huitwa ni haki ambazo binaadamu kuzaliwa nazo”-amesisitiza Jaji Othman.

Onesmo Olengurumwa-Mratibu wa THRDC

Kwa upande wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC),Mratibu wa kitaifa wa mtandao Onesmo Olengurumwa, amesema mawakili hao watapata uzoefu na kuwasaidia wananchi wanapohitaji msaada,kusaidiwa kuendesha mashauri ya haki zinazohusu ubinadamu nazipo kwa mujibu wa kikatiba.

Amesema wananchi wanapaswa kutumia njia za busara kudai haki kwa kwenda mahakamani na sio kwenda barabarani kufanya vurugu hivyo wakipata mawakili wa kuwasaidia watadai haki zao mahakamani.

“Mawakili na wananchi wakielewa vizuri  kudai haki zao kupitia mahakama kutapunguza malalamiko na uonevua”amesema Olengurumwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud, amesema mafunzo hayo ni ya kipekee ambayo yatawasaidia mawakili hao kutetea haki za binadamu.

Amesema kuwa kwa muda mrefu kuna utetezi lakini mawakili  wanafanya kazi zao bila ya kuwa na mifumo na mipango mikakati ya kutetea wanapokua Mahakamani.

“Mafunzo haya yataongeza uwelewa na watakaposimama mahakamani wawe wanafanya utetezi kwa kujiamini na kufuata misingi na taratibu za sheria”alisema.

Alisema hivi sasa kuna mabadilik o makubwa ya sayansi na teknolojia hata watenda makosa wanambinu nyingi hivyo bila kuwa na mafunzo ya mara kwa mara kunasaidia kutuweka pamoja na kujua mbinu za watendaji makosa”alisema Jamila.

Violah Ajok-Muwakilishi wa American Bar Association Africa Mashariki.

Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa mafunzo kama haya yakihusisha visiwa vote vya Unguja na Pemba ambako mara kadhaa kumeripotiwa kuwepo kwa matukio mengi ya ukiukwaji wa Haki za binadamu na hasa kwa wanawake ambapo hata rais wa Zanzibar Dkt. Husein Mwinyi amenukuliwa mara akikiri kushamili kwa vitendo hivyo kwa kundi hilo.