February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC YAONGEZA MKATABA WA KUENDELEA KUFANYA KAZI NA ICNL

Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeongeza mkataba wa kuendelea kushirikiana na shirika la International Center for Non-profit Law (ICNL) toka nchini Marekani. Mkataba huu una thamani ya dola za kimarekani elfu arobaini (USD 40000/=) sawa na shilingi za kitanzania milioni tisini (TSHS 90,000,000/=). Mkataba huu ni kwaajili ya kuimarisha shughuli za utetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi tarehe 15/02/2022 na Utekelezaji wake utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi Februari 2022 na kumalizika Oktoba mwaka 2022.

Fedha hizi zitatumika kuendeleza mchakato wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyokubaliwa na serikali katika tathmini ya baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu Tanzania. Pia zitatumika katika utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa watetezi wa haki za binadamu nchini ikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na waandishi wa habari. THRDC imekuwa ikifanya Kazi na Shirika la ICNL kwa muda mrefu kama Wadau wakubwa wa Haki za Binadamu na Wafadhili wa miradi mbalimbali ya Mtandao.

TRANSLATION

THRDC EXTENDS GRANT AGREEMENT WITH ICNL

The Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) has signed a grant worth USD 40,000 (equivalent to 90 million Tanzanian Shillings) with the International Center for Non-profit Law (ICNL) based in the USA. The grant aim to support and strengthen human rights activities in Tanzania.
The agreement was officially signed on 15/02/2022 and its implementation will commence late February 2021 and run until October 2022.

The funds will be used to facilitate the development of an implementation follow-up strategy for recommendations accepted by the Tanzanian government in the Universal Periodic Review (UPR). Also in strengthening the work of human rights defenders including CSOs and journalists through capacity building trainings.

ICNL has been among the THRDC’s founding partners and a major stakeholder of Human Rights in Tanzania.

Issued by THRDC
24/02/2022