December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC YALAANI TUKIO LA KUKAMATWA KWA WANAHABARI

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamua Tanzania umelaani tukio la kushikiliwa kwa mchora katuni, Optatus Fwema na Mwandishi wa habari wa Mgawe TV, Harlod Shemsanga na kulitaka jeshi la polisi kuwaachilia huru au kuwafikisha mahakamani.

Kauli hiyo imetolewa hii leo katika taarifa iliyotolewa na Mtandao huo kwa wanahabari ambapo wameeleza waandishi hao kuendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi Zaidi ya saa 24 ni Kinyume cha sheria.

Optatus Fwema anayeshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikamatwa na polisi  nyumbani kwake Bunju mkoani Dar es salaam mnamo tar 24 sept 2021 na kuhojiwa kuhusu tuhuma za Makosa ya mtandaoni hata hivyo kwa mujibu wa THRDC imeeleza Fwema alihojiwa bila kuwepo kwa wakili wake au mwanafamilia.

Aidha mwandishi wa habari wa Mgawe tv, Harlod Shemsanga anayeshikiliwa katika Kituo cha Mbweni,alikamatwa Octoba 2,2021 kwa tuhuma za kufanya mazoezi ya kukimbia bila kibali cha polisi, Shemsanga alikamatwa pamoja na wanawake wanachama wa CHADEMA