March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC NA SAVE THE CHILDREN TANZANIA KUENDELEA KUKUZA USHIRIKIANO

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ,leo Machi 25, 2022, umepata furaha, kutembelewa na wawakilishi wa Shirika la Save the Children Tanzania, Bw. Wilbert Mushungusi na Bi. Mariana Kavishe

Katika Ugeni huo timu ya Save the Children na THRDC zimejadiliana mbinu za kuongeza mashirikiano baina yao hasa katika maswala ya kukuza nafasi za Kiraia nchini (Civic Space) katika kipindi cha miaka mitano (5) ijayo (2022- 2026).

Katika mazungumzo hayo, timu ya THRDC imeikaribisha timu ya Save the Children na kuishukuru kwa kutambua umuhimu mkubwa kwa watetezi wa Haki za binadamu kufanya kazi pamoja katika kulinda na kutetea haki za binadamu na kuahidi ushirikiano.

Kwa muda mrefu sasa THRDC imekuwa ikishirikiana na taasisi ya Save the Children katika uratibu wa mchakato wa mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu Tanzania (Universal Periodic Review -UPR) ambao unafanyika kila Baada ya miaka minne na kuleta matokeo chanya katika maswala ya ulinzi na utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.