February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC, LHRC, SAVE THE CHILDREN, PAMOJA NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU, WARATIBU KIKAO CHA WADAU WA NDANI YA NCHI KUHUSU MZUNGUKO WA TATU WA MAPITIO YA HALI YA HAKI ZA BINADAMU (UPR)

Na: Anthony Rwekaza

Serikali imewapongeza wadau wa haki za hinadamu Nchini kwa kuandaa Mkutano wa kujiandaa na mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, ambao utajadili taarifa kuhusu namna Nchi ilivyotekeleza mapendekezo ya masuala ya Haki za Binadamu kwenye mzunguko wa pili wa miaka minne ulioanza kutekelezwa Septemba 2016 na kutoa mapendekezo mapya.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es salaam hapo jana Oktoba 5, 2021, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amepongeza wadau hao ambao ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Save the Children kwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu Tanzania.

Amesema mkutano huo utatoa fursa kwa wadau hao kujiandaa na kuwaeleza mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali juu ya mambo yaliyoingizwa kwenye taarifa yao pamoja na taarifa ya Nchi, kufikiria juu ya vitu ambavyo wanaweza kuviibua ikiwemo mapendekezo ya msingi na yenye matiki ambayo Serikali inaimizwa yaletwe.

“Sisi kama serikali tunapongeza hiki kitu (mkutano) kwa kuwa kinatoa fursa ya wao kujiandaa lakini kueleza hata mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ambao mmeona walikuwepo, juu ya ni nini nini kimeingizwa kwenye taarifa yao, nini kimeingizwa kwenye taarifa ya Nchi, ni vitu gani wanaweza wakaviibua kama mapendekezo ya msingi yenye mantiki na uzito ambayo kimsingi sisi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaimiza walete hayo” amesema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju

Pia Mpanju amesema Baraza la Kimataifa la Haki za Binadamu na kuwekwa kwenye ‘Website’ yao, ambapo ameeleza kuwa taarifa hiyo itajadiliwa Novemba 5, 2021 Mjini Geneva Nchi Usswiz yalipo zilipo ofisi kuu, ambapo amebainisha kuwa Nchi ya Tanzania itatuma wawakirishi watakaoenda kuwasilisha na kujibu hoja zinazoweza kuibuliwa kwenye mkutano huo.

“Hiyo taarifa tayari imeshapokelewa kwenye Baraza la Haki za Binadamu na tayari imeshawekwa kwenye Website yao, na taarifa hiyo itajadiliwa tarehe 5/11/2021, ambako Tanzania tutatuma wawakilishi watakaoenda, kuwasilisha na kujibu hoja mbalimbali zitakazoibuka” amesema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju

Ambapo katika hatua nyingine amebainisha msimamo wa Serikali kuwa Nchi ya Tanzania inazo taratibu zake, Katiba yake, sheria sheria zake, sera mila na tamaduni, hivyo amesisitiza kuwa Serikali inaimiza Nchi zote za Umoja wa Mataifa ambazo zitashiriki kujadili taarifa ya Nchi kuweza kutoa kmapendekezo yaliyo wazi na yanayozingatia Katiba, sheria, sera na mila na Desturi za Nchi, ambapo ameongeza kuwa mzunguko uliopita jumla walitoa mapendekozo 227 huku Serikali iliyakataa mapendekezo 94 kwa sababu mbalimbali huku wakibakia na mapendekezo 133 ambapo 32 kati ya hayo yalikubali baadhi ya vipengele.

Aidha kwa upande wa waandaaji wa mkutano huo Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa ambaye naye alipata fursa ya kuzungumza kwenye mkutano huo ameelezea kuhusu mchakato huo unatambulika kama ‘Universal Periodic Review’. (UPR).

Amesema ni mchakato ambao ufanyika kila baada ya miaka minne ambao upo chini ya Umoja wa Mataifa, kwenye Ofisi za Haki za Binadamu, ambapo utekelezwaji wake unatokana na makubaliano baina ya Umoja huo na Taifa kuwa kila baada ya miaka minne Taifa lipitiwe kupitia mawasilisho ya taarifa kuhusu utekelezaji wa Haki za Binadamu au mapendekezo yanayotokana na mapitio ya awali” amesema Olengurumwa.

“Universal Periodic Review (UPR) ni mchakato wa kila baada ya miaka minne ambao hupo chini ya Umoja wa Mataifa, ofisi ya Haki za Binadamu ambapo walikubaliana kila baada ya miaka minne Taifa linapitiwa kuhusu utekezaji wa Haki za Binadamu au mapendekezo ambayo yalitokana na mapitio yaliyopita” ameeleza Olengurumwa

Lakini pia Onesmo Olengurumwa ambaye ni Mratibu wa mtandao ambao umekuwa ukitetea Haki za Binadamu Nchini Tanzania katika mambo na sakata mbalimbali zinazotokea ambazo utafsiriwa kuwa zinakiuka Haki za Binadamu, amesema kwa miaka minne licha ya Serikali kufanya vizuri kwenye baadhi ya mambo yanayohusu haki za binadamu lakini amedai kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo, uhuru wa kujieleza, uhuru wa taasisi na asasi za kiraia, uhuru wa watetezi wa haki za binadamu pamoja na kutungwa kwa baadhi ya sheria kali, ambavyo amedai kuwa upelekea haki za binadamu kudorola.

“Kwa miaka hii minne Haki za Binadamu kwa namna moja au nyingine haukwenda vizuri zaidi, ndiyo maana kwetu sisi pia tuna ripoti yetu, Serikali wana ya kwao na uzituma kwa pamoja, tuna uhuru wa kuandika kile tulichokiona, kuna maeneo tumefanya vizuri katika haki za binadamu na kuna maeneo hatujafanya vizuri, mfano kwenye maeneo ya uhuru wa kujieleza, uhuru taasisi mbalimbali, uhuru wa asasi za kiraia, watetezi wa haki binadamu, sheria kali kali zilizotungwa, zote zimefanya haki za binadamu zizolote…, tunadhani mapendekezo yatajitokeza sahihi kwamba hayo maeneo yaendelee kuboreshwa zaidi.” Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Vilevile Kaimu Mtendaji Mkuu Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini, Narsor Assey, amesema licha ya mchakato huo ambayo ni mapendekezo kuwa ni jukumu la Serikali lakini hauwezi kukamilika bila kushirikiana na wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu Nchini ikiwemo tume hiyo pamoja na taasisi zinatekeleza majukumu yanayogusa haki za binadamu, huku akisema mkutano huo unasaidia kupeana taarifa za awali ili wakieanda kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la haki za binadamu wawe wanatambua msimamo wa Nchi, ili wakipata fursa ya kuhoji waeleze uhalisia uliopo Nchini kuhusu haki za binadamu.

“Huu mchakato ni mchakato wa Serikali (State Driven or led Process) lakini mchakato huu wa Serikali hauwezi kukamilika kama wadau mbalimbali wa haki za binadamu, ikiwepo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na hizi asasi za kiraia na wadau mbalimbali wa masuala haya hawajashiriki, ndiyo maana tupo hapa leo (kwenye mkutano) kupeana uelewa na kupeana taarifa za awali, kwa sababu unapokwenda kule Geneva kwenye Baraza la haki za binadamu, wanoingia ndani na kuhoji ni mabalozi na wadau mbalimbali wa haki za binadamu, sasa ni vizuri wakaelewa msimamo wa Serikali ya Nchi yetu, hali halisi ya Nchi yetu inavyoendelea na wakati wa kuongea mambo yanayogusa ukweli na uhalisia wa hali ya haki za binadamu Nchini kusikia na kuambiwa bila kusikia kutoka kwetu ambao ni wadau na tunaishi kwenye Nchi yetu” amesema Kaimu Mtendaji Mkuu Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini Tanzania, Nabor Assey