February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

THRDC, KPMG, NA WAJIBU INSTITUTE KWA KUSHIRIKIANA NA TRA WAZINDUA MWONGOZO KUHUSU KODI

Na: Anthony Rwekaza

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), pamoja na asasi nyingine za kiraia kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA wamezindua mwongozo wa asasi za kiraia kuhusu kodi.

Akizungumzia mwongozo huo Feliciana Nkane kwa niaba wa kamishina ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwenye Ofisi za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Kitaifa (THRDC), amezipongeza asasi za kiraia zilizoshiriki kwa pamoja katika mchakato wa kupata muongozo huo.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TRA inatambua umuhimu wa asasi za kiraia katika kuchangia pato la Taifa, kwa kulipa kodi, kuelimisha umma kuendelea kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa

“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa kunialika kushiriki pamoja nanyi kwenye tukio hili muhimu. Siku zote Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) inatambua umuhimu wenu katika kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi kuelimisha umma hivyo kuendelea kuchangia katika maendeleo va taifa” Naibu Kamishna wa TRA Feliciana Nkane

Aidha ameupongeza Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania,Accountability Tanzania, WAJIBU-Institute of Public Accountability kwa kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na TRA kuhakikisha mwongozo huo unakamilika na kuzinduliwa.

“Kwa namna wa pekee napenda kuwapongeza Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Accountability Tanzania, na WAJIBU-Institute of Public Accountability kwa kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na sisi TRA katika kuhakikisha mwongozo huu unakamilika na leo kuzinduliwa” amesema Naibu Kamishna wa TRA, Feliciana Nkane

Aidha amesema kufuatia ushirikiano baina ya TRA na Asasi za Kiraia (AZAKI) ambao amedai umechangia kushirikiana kuandaa mwongozo huo, amebainisha kuwa ni dhairi hatu hiyo itaendeleza ushirikiano ambapo itapelekea kukabiliana na changamoto za AZAKI

“Ni dhahiri kwamba mahusiano yetu yatazidi kuimarika na changamoto zinazohusu kodi katika sekta ya AZAKI zitazidi kupungua, Napenda kutambua mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia (AZAKI)/ Watetezi wa Haki za Binadamu katika pato la taifa” amesema Naibu Kamishna wa TRA, Feliciana Nkane

Vilevile ameupongeza Mtadao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kuendelea pato la taifa kupitia kodi mbalimbali kama vile Kodi ya Mapato (PAYE), Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Withholding Tax (Kodi ya Zuio), ushuruwa stempu (Stamp Duty) na kodi zingine nyingi, pia azipongezanAsasi za Kiraia kwa kuendelea kufanya manunuzi makubwa na pia kutoa huduma mbalimbali.

Katika uzinduzi huo pia Mratibu wa Kitaifa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema Mtandao huo kupitia wanachama wake wamekuwa wakitambua umuhimu wa kodi na amebainisha kuwa THRDC na washirika wake July 2019, kwa kushirikiana na TRA waliandaa warsha na mafunzo ili kukuza uwezo wa Asasi hizo katiaka utekelezaji wa sheria na mingozo ya kodi, ambapo amedai mafunzo hayo yalipelekea utengenezwaji wa rasmu ya mwongozo wa Kodi kwa Asasi za Kiraia.

“Kwa kutambua umuhimu huu, July 2019, THRDC na washirika wake kwa kushirikiana na TRA iliandaa warsha na mafunzo mbalimbali ili kukuza uwezo wa Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali ya kodi. Warsha na mafunzo haya yalipelekea kutengeneza rasimu ya Mwongozo wa Kodi kwa Asasi za Kiraia kama Jarida maalum.” Amesema Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Aidha Mratibu huyo, ameipongeza TRA na washirika wa Mtandao wa mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), kwa kuonesha ushirikiano katika kuandaa Jarida maalum kwa ajili ya kusaidia Asasi za Kiraia, pia amebainisha kuwa chimbuko la mpango huo ulitokea kutokana na mikutano ya wakurugenzi wa Asasi za Kiraia mwaka 2019.

“Kwa namna wa pekee napenda kuwapongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), washirika wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Accountability Tanzania, na WAJIBU-Institute of Public Accountability kwa ushirikiano mlioonyesha katika kuandaa Jarida Maalum (Tool-Kit) kwa ajili ya kusaidia Asasi za Kiraia katika kukuza wa kutekeleza matakwa ya sera, sheria na miongozo mbalimbali kuhusu haki na wajibu wa AZAKI katika kulipa kodi nchini. Mawazo ya kuwepo kwa mwongozo huu yalitokana na mikutano ya warugenzi wa Asasi za Kiraia toka mwaka 2019 mpaka sasa” amesema Mratibu Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Naye Mkurugenzi wa Huduma ya elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo amesema mwongozo huo uliochapishwa kama Jarida, unaweza kufanyiwa marekebisho hasa pale yanapotokea mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazogusa maudhui yaliyoainishwa ili kukidhi maitaji ya wakati husika, huku akisisitiza kuwa wataedeleza ushirikiano ulipo baina ya TRA na AZAKI akitolea mfano Asasi kuendelea kupewa fursa ya kuwasilisha mawazo yao wakati wa mapendekezo ya bajeti na inapotakiwa kufanya mabadiliko ya sheria mbalimbali.

MWISHO