March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

TATIZO LA LUKU, WATATU WASIMAMISHWA KAZI

Waziri wa nishati Merdard Kalemani amemsimamisha Kazi kwa muda wa siku 10 Meneja tehama (ICT) na huduma za biashara wa TANESCO, Lonus Feruz Pamoja na wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau. Ndani ya siku hizo 10 wametakiwa kutoa maelezo kufuatia tatizo la mfumo wa Luku kupitia njia ya kielektroniki na iwapo itashindikana kupatikana maelezo ya kujitosheleza wataondolewa kabisa Kazini.

Kufuatia tatizo hilo lililotokea katika mfumo wa Manunuzi ya Umeme (LUKU) Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwataarifu Wateja wake kuwa, huduma za manunuzi ya LUKU zinapatikana kwenye ofisi za TANESCO za Mikoa na Wilaya, wakati wataalamu wa shirika Hilo wakiendelea na kazi ya utatuzi wa manunuzi kupitia njia za kielektroniki.

Shirika Hilo limeomba radhi na kuwataka Wananchi Kuwa wavumilivu pindi wanapolishughulikia tatizo Hilo.