February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

TARIMBA AKANUSHA TAARIFA ZA KUTAKA WABUNGE WALIPE KODI

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abbas Tarimba amekanusha taarifa inayosambaa katika mitandao ikieleza nia yake ya kupeleka muswada bungeni utakaowataka wabunge wakatwe kodi.

“kuna watu nisiowafahamu wamefungua akaunti Twitter kwa jina langu na kuweka hoja ambayo sio hoja yangu na siifhamu, si hoja ya kujenga bali ya kubomoa,inalenga kunivunjia heshima…ni hoja ambayo inaniharibia na aliyefanya hivi kwa madhumuni ya kuniumiza kweli hii imeniumiza,”