Rais Samia suluhu hii leo ameupokea ujumbe maalum kutoka kwa rais wa Rwanda,Paul kagame uliowasilishwa na Mjumbe maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Dkt. Vincent Biruta.
Marais wa Tanzania na Rwanda wameahidi kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili hususan katika utekelezaji wa miradi ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo na ujenzi wa reli ya kisasa ya kuunganisha Jiji la Kigali na Isaka (Tanzania) ambayo itasaidia katika usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Rwanda.
Rais Kagame kupitia ujumbe huo maalum ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania,Hayati Dkt John Pombe Magufuli na kumpongeza Rais Samia Suluhu kwa kupokea kijiti cha urais
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA