February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

TANZANIA: BEI YA MITUNGI YA GESI YAKUPIKIA MAJUMBANI KIZUNGUMKUTI, YAMUIBUA WAZIRI KALEMANI

Na: Anthony Rwekaza

Licha Nchi ya Tanzania kuzalisha gesi, huku Serikali yake ikisisitiza matumizi ya Nishati za kupikia ili kuepusha uribifu wa mazingira, ikiwepo changamoto ya ukataji miti kwa ajili ya kuni na kuchoma mkaa wa kupikia, lakini hali imekuwa sio shwari kutokana na kuzungumkuti kutanda kufuatia bei ya gesi ya kupikia majumbani kupanda kiholela.

Augosti 3, 2021 Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), baada ya kusikia kilio cha wananchi wengi watumiaji wa gesi majumbani, ilitoa maelekezo kupitia barua iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Godfrey Chibulunje wakilili bei ya gesi kupanda kiholela na walilazimika kwenye barua hiyo kutoa maelekezo ya kampuni yoyote kutopandisha bei badadala yake kama watakuwa na sababu za kufanya hivyo waliwataka kuwasilisha hoja zao kwa EWURA, kinyume na hivyo barua ilidai watachukuliwa sheria kali.

Licha ya maelekezo hayo hali iliendea kuwa vilevile hasa kwa walaji wa mwisho huku bei ya mtungi wa kilo sita ukiuzwa sio chini ya elfu 23, 000, na mtungi wa kilo 15 ukiuzwa sio chini ya elfu 53, hata mitungi mikubwa zaidi nayo bei yake ikiongezeka kulingana na maeneo jambo ambalo lililozidi kuwaweka wananchi njia panda.

Baada ya kilio cha wanatumiaji kuendelea, Waziri Merdadi Kalemani akiwa kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa aliibuka na kuwekea mkazo juu ya kauli EWURA akitaka Makampuni na wauzaji wa gesi kote Nchini kusitisha upandishwaji kiholela wa bei ya kupikia gesi majubani.

Waswahili usema ukisikia mayowe ujue limempata, sauti za wananchi hazikukomea hapo kilio kilizidi kuendelea kwa wananchi ambao wanatumia gesi hasa kwa wafanyabiasha wanaotegemea gesi kuendesha biashara zao hasa watengenezaji wa chipsi kwenye migahawa na wauzaji wa vyakula mahotelini.

Watetezi TV ilibisha hodi kwa Mfanyabiasha mdogo anayefanya biashara ya chipsi maeneo ya Ilala Dar es salaam Juma Said , baada ya kuulizwa kuhusu kupanda kwa mitungi ya gesi ya kupikia, alikili na kudai kuwa changamoto hiyo imekuwa ikimpunguzia faida na biashara imekuwa ngumu kutokana bei ya gesi kuwa juu, huku pia akidokeza na bei ya mafuta ya kula kuwa hipo juu.

” Kwakweli bei ya gesi imepanda hatuelewi ni kwanini, lakini kwangu na marafiki zangu imetupunguzia faida kutokana na kuwa juu tofauti na ilivyokuwa lakini biashara yetu imekuwa ngumu kiujumla maana hata mafuta ya kupikia bei yake hipo juu” amesema mfayabiashara Juma Saidi

Pia mfanyabiashara huyo aliziomba Mamlaka za Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chao kusimamia kushuka kwa bei hiyo ili waweze kuimudu kulingana na kipato chao na ameshauri kwa wanaopandisha bei hiyo kiholela wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Aidha kupanda kwa bei hiyo ya huduma muhimu kwa wananchi kumemuibua tena Waziri wa Nishati, Medard Kalemani ambaye ametoa maelekezo tena ya bei kutopandishwa kiholela, huku akielekeza Makampuni kuwasimamia wateja wao kutopandisha bei licha ya kudai kuwa gesi imepanda kwenye soko la Dunia lakini amesisiriza kuwa hisiwe sababu ya kufanya bei kuwa juu zaidi.

“Maelekezo ninayotoa leo hakuna kupandisha bei, Soko la Dunia bei imepanda, lakini haijapanda kiasi cha kupandisha bei namna hiyo lakini mtungi wa kilo 15 usizidi zaidi ya elfu 47,000/=, kwa upande msambazaji na kwa upande wa muuzaji tumekutana naye tumemwambia asizidi elfu 52,000/=, ishuke chini tunajua imepanda lakini isiende juu” amesema Waziri Nishati, Medard Kalemani

Vilevile Waziri Kalemani amesema amewapa onyo kali watakaobainika wanaendelea kupandisha bei ya gesi hizo ikiwemo kuwafungia vituo vyao, lakini amesisitiza kuwa UWURA wameshatoa maelekezo yanayotakiwa kuzingatiwa .

” Kwahiyo tunapita kuwapa onyo ya mwisho, EWURA wameshatoa maelekezo mimi nimepita kama Waziri, natoa onyo ya mwisho tukija kesho tukakuta bei imepanda tutawachukua na kuwafungia kituo jumla jumla” amesema Waziri wa Nishati, Medard Kalemani

Watetezi TV imebaini kwa kila ukubwa wa mtungi imeongezeka sio chini ya kiasi cha shilingi elfu 3,000/=, kwenye maeneo mengi Nchini tofauti na kipindi cha miezi mitatu iliyopita kabla ya sintofahamu hiyo kuibuka na kuibua gumzo kwa wananchi sehemu mbalimbali Nchini Tanzania.