March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SOMALIA:UCHAGUZI KUFANYIKA NDANI YA SIKU 60

Rais wa Somalia,Mohamed Abdullahi Mohamed

Somalia imetangaza kuwa uchaguzi nchini humo utafanyika ndani ya siku  60 zijazo, uamuzi ambao umetolewa baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya kisiasa yaliyokuwa yakifanyika katika mji wa Mogadishu nchini humo.

Waziri wa Habari, Abdirahman Yusuf  amesema wamekubaliana  kuwa uchaguzi ufanyike ndani ya miezi miwili na tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi itatangazwa na Tume ya uchaguzi hapo badae .Naye Waziri Mkuu wa Somalia,Mohamed Hussein Roble amesema hatua iliyofikiwa ni ya kihistoria.

Uchaguzi nchini Somalia  ulitarajiwa kufanyika mwezi Februari  mwaka huu ukaingiwa na dosari baada ya  serikali inayoongozwa na rais Mohamed Abdullahi Farmajo kushindwa kuelewana na viongozi wa majimbo matano juu ya namna ya kuufanikisha uchaguzi huo na Bunge kupitisha mswada wa kumuongezea Rais Farmajo muda wa miaka miwili suala ambalo lilipingwa na upinzani.