February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SHIRIKA LA WORLD VISION LASHEREKEA MIAKA 40 TOKEA LIAZE KUFANYA KAZI TANZANIA, LAZINDUA MPANGO MKAKATI MPYA

Na: Anthony Rwekaza

Waziri wa Ofsi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu amelipongeza Shirika la ‘World Vision’ kwa kufanya kazi za maendeleo na Serikali kwa kipindi cha miaka 40 tokea lilipoanzishwa, pia amewasilisha salamu za pongezi kwa Shirika hilo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pongezi hizo amezitoa wakati akizungumza akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uzindunzi wa mpango mkakati wa miaka mitano 2021/2025 ulioambatana na maadhimisho ya miaka 40 tokea Shirika hilo lilipoanzishwa mwaka 1981.

Waziri Ummy Mwalimu amesema licha ya pongezi zake lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ambazo amezituma kabla ya hafla hiyo, akiwapongeza Shirika hilo kwa kufanya kazi Tanzania kwa miaka 40, huku matarajio yake kwa Shirika hilo ni kuwa litandelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya awamu ya sita katika kutatua changamoto mbalimbali.

” Niaze kupongeza World Vision…, lakini pia naomba niwasiliehe salamu za pongezi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, amenituma kwamba anafurahi mmekuwa hapa safari ya miaka ya miaka 40 na leo mnaadhimisha miaka 40 na ni matarajio yake kwamba mtaendelea kufanya kazi kwa karibu katika kushirikiana na Serikali yake katika kutatua changamoto hususani zinazohusu maendeleo ya watoto, ustawi wa watoto, wanawake pamoja na jamii” amesema Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu

Pia Waziri Ummy Mwalimu lamesema Serikali imekuwa ikitambua mchango wa World Vision katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Shirika hilo kwenye maeneo mbalimbali Nchini, hususani kwenye Sekta ya kuwezesha miundombinu kwenye jamii zenye uitaji.

” Tumeshudia ujenzi mkubwa wa zanati, nyumba za waganga, usambazaji wa vifaa tiba vyenye gharama kubwa lakini tumeshudia huduma nyingi ikiwemo kuwatua ndoo kichwani wakina Mama, kusogeza karibu huduma za maji, ujenzi wa miundombinu ya maji kama vile wa matanki makubwa ya maji yanayotumia pampu zinazoendeshwa na nishati ya jua” amesema Ummy Mwalimu

Aidha Mkurugenzi wa World Vision Tanzania, Gilbert Kamanga ameipongeza Serikali na wadau kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na Shirika hilo, huku akitaka ushirikiano huo kuendelezwa ili kufanikisha malengo ya mkakati mpya wa miaka mitano 2021/2025 uliozinduliwa Septemba 2, 2021 Jijini Dodoma.

Vilevile Mkurugenzi huyo amesema licha ya Shirika hilo kuwa chini ya Dini Katoriki, lakini limeendelea kutoa huduma kwa Jamii bila kujali madhehebu ya wanufaika, jambo ambalo limepongezwa na Waziri Ummy Mwalimu.

Katiki mpango mpya wa miaka mitano uliozinduliwa rasmi Kamanga amesema umelenga kutoa kuongeza utoaji wa huduma muhimu hasa kwa Watoto hususani katika kupambana na changamoto za elimu kwa kushirikiana na Serikali, pia kuwezesha upatikanaji wa uduma za afya kwenye jamii sambamba na kukuza mitazamo ya jamii kuhusu masuala ya maendeleo.

Ikumbukwe Shirika la World Vision lilianza kufanya kazi rasmi Nchini Tanzania mwaka 1981 chini ya Rais wa awamu ya kwanza Mwl. Julias Kambarage Nyerere kwenye Mkoa wa Dodoma lakini mpaka linatimiza miaka 40 tayari wamefikia Mikoa 18 ambapo wanapanga kukuza huduma mbalimbali za kijamii kwenye Mikoa mingine zaidi.