March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SHINYANGA:AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTIYE

Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga imemhukumu, Petro Maro kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 13.Hakimu Mfawidhi,Ushindi Swalo ametoa hukumu hiyo hii leo katika kesi hiyo ya jinai Na.175/2020.

Shirika la AGAPE ACP limeipongeza Serikali kupitia mamlaka zake, jamii na wadau kwa namna walivyotoa ushirikiano hadi haki imetendeka na kutoa wito kwa jamii kuepuka na kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.