February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SHAHIDI KESI YA WAKINA MBOWE ASEMA AFYA YAKE YAIMARIKA, APANDA TENA KIZIMBANI

Na Antony Benedicto

Baada ya Shahidi wa Jamhuri Innocent Ndowo kupata changamoto ya kiafya iliyopelekea Mahakama kuahirishwa kwa kesi namba 16/2021,hapo jana Jumatatu Januari 17, 2022 ili kumpa nafasi ya kupata matibabu, leo Jumanne Januari 18, 2022 shahidi huyo amepanda tena kizimbani kuendelea kutoa ushahidi baada afya yake kuimarika.

Shahidi huyo ambaye ni shahidi wa 10 wa upande wa Jamhuri anaendelea kuongozwa na Mawakili wa Jamhuri, na mara baada ya kukamirisha hatua hiyo upande wa utetezi unatarajiwa kumuuliza maswali ya dodoso (cross examination) kabla ya hajaitimisha ushahidi wake.

Itakumbukuwa Kesi hiyo yenye mashtaka ya ugaidi inawakabili washtakiwa wanne, ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Khalifan Bwire, Adam Kasekwa, Muhammad Ling’wenya wote hao wamefikishwa Mahakamani.