February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SERIKALI YAPANGA KUZIFANYIA MAPITIO SHERIA ZA HABARI ZINAZOLALAMIKIWA NA WADAU

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema katika bajeti ya mwaka mpya wa fedha 2022/2022 unakaribia kuanza hivi karibuni inatarajia kufanya mapitio ya sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya huduma ya Habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.
Akizungumza Mei 20, 2022 Bungeni Jijini Dodoma katika mawasilisho ya mapitio na mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo, Waziri mwenye dhamana Nape Nnauye amesema kuwa katika mwaka huo wa fedha Serikali inapanga kufanya mapitio kwenye sheria mbalimbali zinazogusa sekta ya habari.
“Serikali inapanga kufanya mapitio ya Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003 ili kuifanya iendane na mabadiliko katika Sekta ya Habari, pia inapanga kufanya mapitio ya baadhi ya vifungu katika Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 na Kanuni zake za Mwaka 2017″amesema Nape.
Pia Waziri Nnauye amesema kuwa kupitia Idara ya Habari Maelezo Wizara hiyo itaendelea kuchapa na kutoa leseni za magazeti na vitambulisho vya waandishi wa Habari.
Ameongeza kuwa katika mwaka huo wa fedha 2022/2023 Wizara inapanga kutoa miongozo na kufanya tathmini ya utoaji taarifa kwa umma kwa kila Taasisi, huku akisema kuwawamepanga kusimamia utekelezaji wa Sera ya Habari na Utangazajiya Mwaka 2003, Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 na Kanuni zake za Mwaka 2017 ili kuhakikisha maadili na uzingatiwaji wa Sheria katika Tasnia ya Habari.
Katika jitihada za kuitangaza Nchi Kimataifa amesema kuwa wanapanga kuhasisha vyombo vya nje katika kuitangaza Tanzania, lakini amesema katika bajeti hiyo wanapanga kuanzisha kipindi maalumu cha ‘Ongea na Waziri’ na ujenga studio maalum kwa ajili ya pipindi vya moja kwa moja vya redio na runinga.
“Tunapanga Kuhamasisha Vyombo vya Habari vya nje ya nchi katikakuitangaza Tanzania,kuanzisha kipindi Maalum cha Ongea na Waziri, na kujenga Studio maalum kwa ajili ya Vipindi vya Moja kwa moja vya redio na runinga, miradi itakayotekelezwa na Wizara” ameongeza Nape.
Itakumbukwa Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza Waziri Nape Nnauye kuzipitia sheria ambazo zimekuwa zikikamilikiwa na wadau wa tasnia ya habari ili kama kuna sehemu zinaitaji kufanyiwa maboresho yaweze kufanywa, na tayari kwa mara kadhaa Waziri Nape Nnauye amekuwa akieleza juu ya serikali kuwa jambo hilo tayari wameanza kulifanyia kazi ili kukuza tasinia hiyo.