February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SERIKALI YAKANUSHA UZUSHI WA KILA MTUMISHI WAKE KULAZIMISHWA CHANJO YA CORONA

Kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshaji zilizodai kuwa ni lazima kila mfanyakazi wa Serikali kupatiwa chanjo ya Corona, Upotoshaji huo umemuibua Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye amepinga taarifa hizo na kutoa msimamo wa Serikali.

Gerson Msigwa amesema taarifa hizo zinapotosha jamii amebainisha kuwa Serikali amlazimishi mfanyakazi yoyote wa Serikali kuchoma chanjo ya UVIKO-19 ama ugonjwa wa Corona wala Serikali haijatoa maelekezo yoyote ya kuwalizimisha kupatiwa chanjo na wakienda kinyume wataondolewa makazini.

” Kumekuwepo na taarifa za upotoshaji kwamba Serikali imetoa maelekezo kwamba wafanyakazi wote wa Serikali lazima wapatiwe chanjo ya UVIKO-19 ama ugonjwa wa Corona, napenda kusema taarifa hizo ni za upotoshaji, Serikali haijatoa maelekezo ya kuwalazimisha wafanyakazi wote wapatiwe chanjo na kwamba wasipopatiwa chanjo wataodolewa makazini, maelekezo hayo hayajatolewa na Serikali”amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Aidha Gerson Msigwa katika msimamo rasmi wa Serikali alioueleza ni kwamba chanjo hiyo itatolewa kwa hiari isipokuwa imetoa kipaumbele kwa makundi ambayo yapo hatarini kuathiliwa na janga hilo kama inavyoelezwa na wataalamu wa afya.

“Serikali ilichokisema mpaka sasa ni kwamba chanjo itatolewa na mtu atapokea chanjo kwa hiari yake hisipokuwa yametolewa makundi ambayo yatapatiwa kipaumbele katika kupokea chanjo na makundi hayo ningependa kuyarudia, wafanyakazi kwenye sekta ya afya, madaktari, wauguzi watapewa kipaumbele lakini kundi lenye watu wenye umri zaidi ya miaka 50 ambao ni moja ya makundi hatarishi tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya hao pia watapatiwa kipaumbele” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Tanzania imeanza kutoa chanjo ya Corona kwa raia wake na tayari baadhi ya viongozi kwenye ngazi za juu wamepatiwa chanjo hiyo, miongini mwao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima, Mkuu Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro na wengineo.