February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SERIKALI YAIAGIZA HESLB KUFUTA TOZO KWA WANUFAIKA

Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  imeiagiza  Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  kuondoa tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022

Aidha ameongeza kuwa ifikapo Julai mosi mwaka huu serikali itaondoa tozo ya asilimia ya kulinda thamani ya fedha iliyokuwa ikitozwa kwa wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya juu ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu alilolitoa siku ya Wafanyakazi,Mei mosi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Mikopo Kifungu cha 7(2)(1)(1) cha Mwongozo wa Utoaji wa Mikopo na Ruzuku kinaaisha kuwa mnufaika wa Bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu mnufaika atakapoanza kupokea mkopo, suala ambalo wanufaika wa Bodi ya mikopo,watetezi wa Haki za Binadamu,wanasiasa na Chama vya wafanyakazi walikuwa wakililia kuondolewa kwa tozo hiyo kwani kunaondoa dhana ya kutoa mikopo hiyo kwa watoto masikini.