February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SERIKALI YAANZA KUPITIA MWENENDO WA JESHI LA POLISI, YATAJA CHANZO CHA MAUAJI

Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amesema Serikali inafanyia kazi maelekezo ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), ya kupitia upya mwenendo wa Jeshi la Polisi.

Mhandishi Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, jijini Dar es Salaam, akitoa taarifa ya mafanikio ya wizara yake kwenye kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, madarakani.

Baada ya kuulizwa Serikali imechukua hatua gani juu ya maelekezo hayo, yaliyotolewa hivi karibuni na CCM, ikidai kuna malalamiko kutoka kwa wananchi ya kuwa utendaji wa Jeshi la Polisi hauridhishi kwa kuwa baadhi ya maofisa na askari wanakwenda kinyume na miongozo ya utendaji kazi zao.

“Kuhusu kauli ya CCM kwa  Serikali, ni kujibu kwa ufupi kwamba, kauli ya kamati kuu ya CCM ni maelekezo mimi ni nani nainze kuhoji maelekezo ya chama?  Ninachoweza kuwahakikishia wananchi ni  kwamba maelekezo hayo Serikali imeyapokea na yanaendelea kufanyiwa kazi hatua kwa hatua,” amessma Mhandisi Masauni.

Akizungumzia kuhusu wimbi la matukio ya mauaji lililoibuka nchini hivi karibuni, Mhandisi Masauni amesema chanzo chake ni sababu za kibinafsi.

“Tulishuhdia wimbi la mauaji nchi nzima mfululizo, katika kipindi hususan Januari. Kama mtakumbuka mauaji hayo yalikuwa yanajitokeza kwa sababu ambazo ni za kijamii zaidi, kama nitakuwa sahihi kwamba ukiangalia vyanzo vya mauji hayo, mengi yalitokana na sababu za kibinafsi au za kijamii. Mfano mengine yalikuwa yanasabishwa na kugombania mali, wivu wa mapenzi, ushirikina na ulevi uliopindukia,” amesema Mhandisi Masauni.

Amesema, kufuatia mauaji hayo iliundwa tume ya kuchunguza sababu zake, ili kutoa ushauri kwa Serikali juu ya namna ya kuyadhibiti, ambayo imeshafanya kazi  na mapendekezo iliyotoa yameanza kushughulikiwa.

Mhandisi Masauni amesema, ili kudhibiti mauaji hayo, Serikali itahakikisha kunakuwa na Askari Polisi wa kutosha katika maeneo ya chini

Akielezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, Mhandisi Masauni amesema imeajiri Askari 6,023 na kuwapandisha vyeo  26,464, wa majeshi yaliyochini ya wizara yake.

Amesema katika kipindi hicho, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia taasisi zake, imekusanya maduhuli ya Serikali kiasi cha Sh. 235 bilioni,ambapo wizara yenyewe imekusanya Sh. 329 milioni, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa-NIDA (Sh. 20 bilioni), Jeshi la Polisi  (Sh. 61.5 bilioni), Jeshi la Uhamiaji (Sh. 127 bilioni) na Jeshi la Magereza (Sh.110 milioni).