February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SERIKALI YAAHIDI MAZINGIRA RAFIKI KWA AZAKI, YAACHA WAZI MLANGO WA MARIDHIANO

Waziri wa Katiba na Sheria, George George Simbachawene amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi za kiraia katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanyika huku akizihakikishia kuwa Serikali hipo tayari kutoa ushirikiano kupitia maridhiano endapo kutakuwepo na jambo ambalo linaweza kuwa kikwazo.

Akizungumza Visiwani Zanzibar katika kufunga mkutano wa taasisi zisizo za Kiserikali (AZAKI), uliofanyika kwa siku tatu kuanzia kuanzia March 12, hadi leo march 14, 2022 ukibebwa na kauli mbiu isemayo “Boresha Ushirikiano Kati ya Serikali na Asasi za Kiraia kwa Mendeleo ya Zanzibar”, Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali dhamira ya Serikali ni kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa asasi za kiraia kutekeleza majukumu yake, lakini ameweka wazi kuwa Serikali ipo tayari muda wote kufanya kazi na asasi hizo na endapo kuna changamoto wako tayari kukaa pamoja kutafuta suluhu kwa manufaa ya wananchi ambao ndiyo wanufaika wakuu.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ya utekelezaji wa shughuli zenu za kiasasi, nipende kuaidi kuwa wakati wote milango ya itakuwa wazi endapo kuna jambo mtaiji kutushirikisha, au katika utekelezaji wa majukumu yetu tumebaini kuna jambo halipo sawa, basi msisite kuja tuzungumze kwa sababu maridhiano yanatujenga na kumnufaisha mwananchi ambaye ndiye mnufaika mkubwa na ndiye msingi wa uwepo wenu” amesema Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene

Pia Waziri Simbachawene amesema kuwa kuwa kwa kipindi cha hivi karibuni asasi za kiraia zimekuwa na jitihada mbalimbali zenye tija kwa wananchi ikiwemo ushiriki katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya na elimu pamoja na kukuza haki za binadamu na kuwa waangalizi muhimu katika uvunjaji wa Sheria.

“Kwa kipindi cha hivi karibuni tumeshudia ongezeko la jitiahada mbalimbali za asasi za kiraia zenye manufaa makubwa kwa Wananchi, jitahada hizi ni pamoja na kuimarisha sekta ya elimu kwa kukarabati na kujenga miundombinu mbalimbali ya shule kama vile madarasa, kuimarisha sekta ya afya kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba na ujenzi wa miundombinu ya hospitali, kukuza haki za binadamu na kuwa waangalizi muhimu katika uvunjaji wa sheria” amesema Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene

Ameongeza kuwa kwa kipindi kirefu sasa asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Nchi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, kutokana na umuhimu wake katika masuala ya maendeleo, ambapo amesema kuwa taasisi hizo zimefanya kazi na kukubalika pande zote mbili za muungano yaani Tanzania bara na visiwani Zanzibar licha ya kwamba uratibu wa taasisi hizo kutokuwa suala la muungano.

Hata hivyo Waziri Simbachawene amesema licha ya sheria na ofisi za usimamizi wa asasi hizo kuwa tofauti baina ya Tanzania bara na Zanzibar lakini amedai kuwa maudhuhi ya Sheria mbalimbali zinazosimamia pande hizo mbili zimekuwa zikifanana hususani katika eneo la usimamizi, uratibu na utaratibu wa utendaji wa asasi hizo.

“Lakini ukisoma Sheria zote mbili zinazosimamia asasi za kiraia, yaani Sheria ya Jumhiya no. 6 ya mwaka 1995 kwa upande wa Zanzibar kwa Sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali no.24 ya mwaka 2002 kwa upande wa Tanzania bara, utabaini kuwa sehemu kubwa ya maudhui ya Sheria hizi hususani katika eneo la usimamizi, uratibu na utaratibu wa utendaji wa asasi hizi yanafanana sana, hii inapelekea hata majukumu ya Ofsi ya mrajisi wa asasi za kiraia Zanzibar na Ofsi ya Msajili wa NG’O Tanzania bara kuwa na majukumu yanayofanana juu ya asasi hizi” amesema Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene

Aidha amesema kuwa Serikali zote mbili ya Muungano zina malengo yanayofanana katika kuziratibu na kuzisimamia asasi za kiraia, ambapo amesema kuwa Serikali hizo zinatambua umuhimu wa kufanya kazi na asasi za kiraia kwa lengo la kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, na kuwaondolea changamoto za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazowakabili, lakini pia kufanikisha maendeleo kwa wananchi ambao amedai kimsingi ndio wanufaika wakubwa wa ushirikiano huo.

Itakumbukuwa hivi karibuni Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) ambao ni miongoni mwa asasi zaidi ya 100 zilizoshiriki ikiwa na ofsi visiwani Zanzibar, waliingia makubaliano na Mahakama ya Zanzibar katika upitiaji wa meneo yenye changamoto kwenye masuala ya upatikanaji na utoaji wa haki na kuandaa mpango kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kukuza myororo wa haki visiwani humo.