February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SAKATA LA WABUNGE 19 KUNG’OKA BUNGENI KIZUGUMKUTI, SPIKA TULIA ASEMA ANAIACHIA MAHAKAMA

Licha ya kupokea barua ya kuwafukuza unachama wabunge wa viti maalumu 19(wanaodi kuwa ni Chadema) Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema hawezi kutangaza kuwa nafasi 19 za Wabunge hao ziko wazi, hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi, akidai kuwa wamekata rufaa ya kupinga uamuzi.
Akieleza hayo Bungeni leo Mei 16, Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.
Ameeleza kuwa kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea na hivyo kuwa Wabunge hao 19 wamepeleka kesi mahakamani.
Pia amesema kuwa Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wabunge 19 wa Chadema.
Aidha Spika Tulia ameongeza kuwa Mei, 13, 2022 barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwake kwa mkono na baada ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.
Kufuatia maelezo hayo amesema kuwa mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake, amesisitiza kuwa kama kuna maswali yoyote kuhusu wabunge hao aulizwe yeye.