Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini yameishauri serikali kufungua milango ya kupata ushauri na maoni kuhusu mgogoro wa Ngorongoro kutoka kwa wadau wa Asasi za Kiraia ili kuwezesha upatikanaji wa mapendekezo huru juu ya namna bora ya kutatua mgogoro huo.
Katika tamko hilo lililotolewa hapo jana na kutiliwa saini na AZAKI 14,ambazo zimeahidi kutoa ushirikiano kwa serikali huku yakionyesha hofu juu ya uwepo wa watu waliandaliwa kuonana na Waziri Mkuu tofauti na AZAKI za umoja huo.
“kuna tetesi kuwa kuna watu wanaoandaliwa kuonana na Waziri Mkuu ambao
tunaamini hawataleta maoni huru yaliyotokana na umoja wa mashirika yasiyo ya kiserekali.
Hivyo, tunatahadharisha kuwa hao hawatakuwa ni wawakilishi wa umoja wa mashirika
haya na hivyo maoni yao yachukuliwe kama binafsi nasio kwa niaba ya mashikrika yasio ya
kiserikali”imeeleza taarifa hiyo.
Aidha wamedai kuwepo kwa vikwazo kwa baadhi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yalikwenda kukusanya maoni Ngorongoro ikiwemo kutakiwa kuwa na Kibali maalum kutoka Wizara ya TAMISEMI cha kuwaruhusu kufanya hivyo, wakieleza wapo kuisadia serikali ili kuweza kutoa maamuzi sahihi.
“Tunashauri asasi za kiraia zisitakiwe kuwa na vibali kwenda Ngorongoro kukusanya maoni
ya viongozi wa serikali na wananchi na pia kujionea wenyewe yanayosemwa na magazeti.
Tamko hili linakuja ikiwa ni wiki chache baada ya Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kukusanya maoni na kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro na Loliondo ambapo AZAKI hizi zimeshauri kuwa maamuzi yatakayotolewa na serikali kuhusu Ngorongoro yazingatie utu, haki za binadamu na utawala wa kisheria.
“Kutokana na uzito wa jambo hili,Waziri Mkuu atoe muda wa kutosha kwa mashirika katika kipindi cha mazungumzo na mashauriano ili kuwezesha upatikanaji wa maoni mengi na mapendekezo wa namna bora ya kutatua mgogoro wa Wilaya ya Ngorongoro. Pia kuwezesha serikali kupata muda wa kuchambuwa na kutoa maamuzi stahiki kwa maisha ya wenyeji wa Wilaya ya Ngorongoro na Taifa zima,”imeongeza taarifa hiyo
Kwa upande mwingine Asasi hizo zimesema . Waziri Mkuu atoe maelekezo kwa wasaidizi wake pasiwepo na vitisho, uzuiaji wa kuingia katika eneo la mkutano kwa makundi mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari hususani wa vyombo vya habari binafsi, waandishi wa kujitegemea na Mashirika yasiyo ya kiserikali.
“tunataka uwakilishi wetu tuliouidhinisha katika umoja wetu na pasiwepo na mtu
mmoja, wawili au kikundi cha watu watakao toa maoni kama mashirika binafsi bila kuwa
sehemu ya umoja wa mashirika haya yasio ya kiserikali kwani huweza kupotosha na kutoa
taarifa zisizo sahihi na kupelekea ushauri wa Serikali kutokuwa na mashiko katika kutoa
usuluhishi wa mgorogoro huo,”
Pamoja na hayo Asasi hizo zimesema zipo tayari kushirikana na serikali katika kukusanya maoni na kutoa mapendekezo yao ili waweze kuisadia serikali wakati wa kufanya maamuzi kuhusu mgogoro huo,pia wameiomba serikali kutoa maelekezo ya kutokuwepo kwa vitisho au uzuiaji wa kuingia katika maeneo ya mkutano kwa makundi mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari wa vyombo binafsi.
Sakata la Ngorongoro linazidi kuchukua sura mpya ambapo baada ya Ziara ya Waziri Mkuu kufanyika katika Wilaya ya Ngorongoro na Loliondo ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mgogoro huo, bado wakazi wa eneo hilo wameendelea kudai kuwa ziara hiyo imezidi kuchochea hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo huku wakidai kuwa mchakato wa ufanyikaji wa kikao katika Wilaya ya Ngorongoro ulikuwa tofauti na Loliondo kwani baadhi ya wawakilishi wa wananchi na waandishi wa habari walizuiwa kuingia katika kikao hicho.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA