Rais Hakainde Hichilema wa Zambia ameendelea kuwa gumzo,baada ya hapo jana kusafiri kwa ndege isiyo ya Serikali (Qatar Airways),akiwa na ujumbe wa watu watatu,akiwemo mlinzi wake,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa,unaofanyika New York,Marekani.
Waliosafiri na Rais huyo ni Waziri wa Mambo ya Kigeni wa nchi hiyo,Stanley Kakudo,na Waziri wa Fedha na Mipango,Dr. Situmbeko Musokotwane.
Akiagana na maafisa wandamizi wa serikali yake katika Uwanja wa ndege wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka,Rais Hichilema amesema atawasilisha vyema maono yake juu ya wananchi wa Zambia.
Rais Hichilema pia anatazamia kushiriki katika Mkutano wa juu zaidi kujadili masuala ya Nishati,Chakula,pamoja na janga la Corona,maarufu kama 2021 SDG.
Akiwa na ujumbe wake ,ataikia mwaliko aliopewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na baada ya hapo wataabiri hadi Washington DC ambako atakutana na Makamu wa Rais wa Marekani,Kamala Harris,na baadae atakutana na viongozi waandamizi wa Shirika la Fedha duniani (IMF),kabla ya kurejea nchini kwake,Septemba 27.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Rais huyo nje ya nchi,tangu achaguliwe kuwa Rais mwezi Agosti mwaka huu,akimshinda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo,Edgal Lungu.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS