February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

SABAYA NA WENZAKE WASHINDA RUFAA; JAJI ABAINI USHAHIDI BATILI

Na: Anthony Rwekaza

Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwa sababu mbalimbali kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.

Akitoa uamuzi rufaa hiyo leo Mei 6, 2022 Jaji Sedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo hususani kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Pia Jaji huyo baada ya kutoa uamuzi huo amesema washtakiwa hao Sabaya na wenzake watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.

Hatua ya hukumu hiyo imekuja kufuatia washtakiwa hao kukata rufani namba 129, katika kesi ya jinai iliyokuwa inamkabili Ole Sabaya na Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao ni Silvester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya unyang’anyi kwa kutumia silaha.

Baada ya kukata Rufaa hiyo, mnamo Februari 14, 2022 mahakama ilianza kusikiliza hoja 14 ziliziwasilishwa 14 na waleta rufani, ambazo zilijikita katika kupinga adhabu ya hukumu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha mnamo Oktoba 15, mwaka 2021, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo.

Mawakili wa upande wa wapeleka rufani katika kesi hiyo, walikuwa ni Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa, Majura Magafu, Edmund Ngemela, Silvester Kahunduka na Fridolin Bwemelo, ambao awali walikuwa kwa wakati tofauti walikuwa wakiwatetea washtakiwa hao kwenye kesi iliyopelekea kukatia Rufaa hukumu.

Pia upande mawakili wa Serikali ambao ni upande wa wajibu rufani, waliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofmedy Mtenga, Wakili wa Serikali, Baraka Mgaya na Wakili wa Serikali, Veridia Mlenza.

Itakumbukwa awali wakati hakumu hiyo ikitolewa Mahakamani na Hakimu Amworo, alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani huko, mahakama imewatia hatiani washtakiwa na kuwahukumu miaka 30 kwenda jela kwa kutenda makosa matatu.

Alieleza kuwa makosa hayo unyang’anyi wa makundi pasipo kutumia silaha kosa alibaini kufanywa na washtakiwa wote kwa pamoja, pia kosa lingine ambalo lilielezwa na Hakimu kupelekea kutiwa hatiani ni kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambalo washtakiwa hao, walimtendea Bakari Msangi, kwa kumpiga, kumfunga pingu, kumtishia silaha na kabla kumpora fedha Sh. 390,000 kinyume na sheria.

Sabaya na wenza alifikishwa mahakamani h kwa mara ya kwanza Juni 4, 2021 ikiwa ni baada ya kukamatwa Mei 27, 2022 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumtengua kwenye nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Hai kupisha upelelezi juu ya madai ya tuhuma mbalimbali alizokuwa akihusishwa nazo.

Hata hivyo Sabaya pamoja na Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, amabapo hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Mei 31, 2022.