Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje (karantini) kwa muda wa siku 10.kuanzia Julai 17-28,2021.Marufuku hiyo imewekwa katika mji mkuu wa Kigali na wilaya zingine nane baada ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa covid-19 kuongezeka.
Aidha biashara, shughuli za umma,usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa huku mazishi yakitakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.Aidha watu manaruhusiwa kutoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya huduma muhimu pekee au wafanyakazi muhimu.
Maofisa wa afya nchini humo wamesema kuwa kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta kunafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya.Mpaka sasa taifa hilo lina visa Zaidi ya 50,000 ya maambukizi.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS