March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RIPOTI YA LHRC YAONESHA NAMNA USHIRIKINA ULIVYOCHOCHEA MAUAJI NCHINI 2021

Kituo cha Sheria na Haki za binadamu Nchini Tanzania (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wengine leo Aprili 11, 2022 kimefanya uzinduzi wa ripoti ya 20 ya Haki za Binadamu Tanzania, (TANZANIA HUMAN RIGHTS REPORT 2021), ambapo imetaja baadhi ya mambo ambayo yamechangia maauji nchini Tanzania kwa mwaka 2021 ikiwemo imani za kishirikina.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema mauaji yanayotokana na kujichukulia sheria mkononi kwa mwaka 2021 yameongezeka kwa 6.8% ikilinganishwa na matukio ya mwaka 2020, huku imani za kishirikina akizitaja kuwa zimechochea mauaji kwa 38.4%.

“Mauaji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi yaliongezeka kwa 6.8% ikilinganishwa na mwaka wa 2020, wakati mauaji yaliyochochewa na uchawi au imani za kishirikina yaliongezeka kwa 38.4%.”amesema Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga

Itakumbukuwa hivi karibuni kumekuwepo na wingi wa kuripotiwa kwa matukio mengi ya mauaji pamoja na baadhi ya watu kudaiwa kujiua, hali ambayo ilipekea mijadala mbalimbali kwenye vyombo vya habari pamoja na kuelezwa na rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye baadhi ya hotuba zake.