February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS WA ZAMANI WA AFRIKA KUSINI AKANA TUHUMA ZA UFISADI ZINAZOMKABILI

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekana mashitaka yanayomkabili ikiwemo mashitaka ya rushwa ulaghai na utakatishaji fedha pamoja na mpango wa ununuzi wa silaha wa kiasi cha dola bilioni 2 wakati akiwa rais.

Zuma pia anakabiliwa na tuhuma za ufisadi ambapo anadaiwa kupokea rushwa ya Dola 34,00 kila mwaka kutoka katika kampuni moja ya Ufaransa inayouza silaha inayoitwa Thales ili aiepushe kampuni hiyo dhidi ya uchunguzi kuhusu biashara hiyo lakini Katika utetezi wake Zuma amedai kuwa yeye ni muathirika wa kampeni za kisiasa zilizofanywa na kikundi pinzani ndani ya Chama Tawala cha ANC ambazo zililenga kumchafua.

Hata hivyo Mawakili wa Jacob Zuma wamemtaka mwendesha mashitaka wa serikali,Billy Downer aondeolewe katika kesi hiyo kwa madai ya kuwa hana mamlaka ya kuendesha kesi hiyo na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chombo cha habari cha RFI upande wa mashitaka umeomba muda ili  kujibu ombi hilo na uamuzi utafanywa Julai 19.