March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS WA TLS, DKT. HOSEAH ATOA NENO KUKAMATWA KWA MBOWE NA WENZAKE

“Kufanya kongamano haijawahi kuwa kosa la jinai kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.

Katiba yetu ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria.

Kitendo cha kumkamata usiku wa manane Mheshimiwa Freeman Mbowe na wenzake, kwa sababu ya kuandaa kongamano ni ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi yetu.

Ikiwa kuna tuhuma nyingine dhidi yake bado kwa sheria zetu alipaswa kuwa amefikishwa kwenye mamlaka za kisheria na si kuendelea kuzuiliwa.

Natoa mwito kwa mamlaka kumwachia huru kwa sababu kuendelea kumshikilia ni kukiuka utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

Chama cha Mawakili wa Tanganyika tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu suala hili na tutatoa msimamo wetu na mwelekeo baada ya mashauriano kufanyika kupitia Baraza la Uongozi” Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) Dkt. Edward Hoseah