Rais wa Mali Bah N’Daw na Waziri Mkuu,Moctar Ouane wametangaza kujiuzulu katika nyadhifa hizo hapo jana wametangaza kujiuzulu wakiwa katika Kambi ya Jeshi wanakozuiliwa.
“Tulipofika, walisoma barua yao ya kujiuzulu ambayo ilikuwa tayari imeandikwa,” kimesema chanzo cha kidiplomasia ambacho kilichoshiriki kwenye mkutano wa utatuzi wa mgogoro huo na kubainisha kuwa huenda wawili hao walijiuzulu kwa kulazimishwa.
Viongozi hao wa Mali wanazuiliwa na viongozi wa Mapinduzi katika kambi kuu ya jeshi la nchi hiyo tangu walipokamatwa siku ya jumatatu huku timu ya upatanishi tangu siku ya Jumanne imekuwa ikijaribu kutafuta njia ya kutatua mgogoro huo.

Kwa mujibu wa taarifa Wanajeshi wa CNSP wanaeleza kuwa hawajaridhishwa na serikali mpya iliyoundwa na kutangazwa siku ya jumatatu ambapo maafisa wawili wa Jeshi hilo hawajarejeshwa katika nafasi zao walizokuwa wakishikilia katika serikali ya awali.
Kulingana na chanzo hicho cha kidiplomasia, mkuu mapinduzi ambaye pia ni makamu wa rais wa sasa Assimi Goïta ametangaza kuwa atashikilia nafasi ya rais wa mpito, na nafasi ya makamu wa rais itabaki wazi. Kanali Goïta amesema kwamba amewafuta kazi viongozi hao akiwashhtumu kwa kuunda serikali mpya bila kushauriana naye wakati yeye ni makamu wa rais anayesimamia masuala ya usalama.

Rais aliyejiuzulu na Waziri Mkuu wake, wanatarajiwa kuachiliwa leo jioni pamoja na wafungwa wengine wanaoshikiliwa pamoja.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS