March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS WA BURUNDI KUZURU KENYA

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na mkewe,Angelina Ndayubaha hii leo  anaanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya na  ziara hiyo itaanzia mjini Kisumu.

Taarifailiyotolewa na  ya Ikulu ya Kenya, Rais Ndayishimiye atashiriki katika zoezi la uzinduzi wa miradi mbalimbali ya serikali katika kaunti ya Kisumu na atakuwa mgeni wa heshima wakati rais Uhuru Kenyatta atakapoongoza taifa hilo katika kuadhimisha sherehe za 58 za Siku ya Madaraka zitakazofanyika katika uwanja mpya wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.