March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS SAMIA: SERIKALI YANGU ITAEDESHWA KWA MATENDO MAKALI SIO MANENO MAKALI YAKUVUNJIANA HESHIMA

Na: Anthony Rwekaza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itaendeshwa kwa matendo makali yasiyotumia nguvu kuliko kutumia maneno makali ya yanayoweza kupelekea kuvunjiana heshima.

Akizungumza Ikulu Jijini Dodoma kwenye hafla ya kuwaapisha Mawaziri wapya na Mwanasheria Mkuu wa aliowateua Septemba 12, 2021, amesema Serikali yake kwa sasa itafanya kazi kwa matendo makali ambayo amedai hayatatumia nguvu, amedai kwa kuwa watumishi wengi ni watu wazima atatumia njia ya kufoka ambayo amedai kuwa haileti heshima.

“Tunapokwendea huko, serikali yetu itaendeshwa kwa matendo makali, na si maneno makali. Msinitegemee kukaa na kuanza kufoka hapa nadhani sio heshima, najua wote ni watu wazima wanajua zuri na baya, msitegemee nitafoka, nitafoka kwa kalamu” Rais Samia Suluhu Hassan

Pia Rais Samia amebaisha kuwa kwenye kipindi cha miezi sita ya ambayo imepita tokea alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekuwa mkimya akiwasoma nikiwasoma mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao, huku akidai kuwa naye wapo walikuwa wanamsoma lakini wapo waliouchukulia ukimya wake kuwa ni udhaifu.

“Katika kipindi cha miezi sita cha urais wangu nilikuwa ni mkimya, nikiwasoma mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao, wakati mimi nawasoma na wao walikuwa wananisoma, wapo waliokuwa wanachukulia upole na ukimya wangu kama udhaifu” Rais Samia Suluhu Hassan

Kufuatia hatua hiyo Rais Samia amesema ataendelea kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri na idara nyingine ndani Serikali ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji, huku akiwahasa Mawaziri walioapishwa na wengine ambao wameendelea kukaa kwenye nafasi zao kuendelea kuchapa kazi na kutatua changamoto kwenye wizara zao.

Mawaziri walioapishwa ni Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, akichukua nafasi ya marehemu Elias Kwandikwa, Dkt. Ashatu Kijaji ameapishwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambae uteuzi wake umetenguliwa, January Makamba anachukua nafasi ya Merdard Kalemani kwenye Wizara ya Nishati, Makame Mbarawa amechukua nafasi ya Chamuriho Wizara ya ujenzi na uchukuzi, huku Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan amewaelekeza wakuu wa Mikoa wote Nchini kuwapanga upya wamachinga wote ambao wameonekana kufanyia biashara zao kwenye maeneo yasiyostaili hususani wale ambao wanafanyia biashara zao mbele ya maduka rasmi jambo ambalo ameletaja kuwa linaikosesha Serikali mapato, huku akiwataka Wakuu hao kutumia njia rafiki kuwapanga sio kutumia nguvu.

Ikumbukwe kumekuwepo na hali ya sintofahamu kufuatia baadhi ya viongozi kwenye ngazi za Serikali wakiwemo baadhi ya wakuu wakiwataka wamachinga kuondoka kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye njia za watembea kwa miguu na wanapanga bidhaa zao kwenye maeneo ambayo ni barabara jambo ambalo lilidaiwa kuwa linaweza kupelekea ajari zinazoweza kuzuilika,

lakini pia sintofahamu hiyo hipo kwenye mijadala hasa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya wadau wenye mawazo msetonwakidai kuwa utaratibu wa kwaruhusu kulipia vitamburisho umechangia kadhia hiyo hasa kwenye maeneo ya miji, huku wengine wakiwa na mtazamo sambamba na Rais Samia kuwa wapangwe upya lakini umakini uwepo kwa sababu kundi hilo ni kubwa na lina ushawishi hasa kisiasa na kiuchumi.