Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amesema Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Manedneleo CHADEMA,Freeman Mbowe kwa kipindi kirefu hakuwepo nchini na huenda alijua atakabiliwa na mashitaka ya ugaidi hivyo alivyorudi nchini alianzisha maadamano ya Katiba ili atakapokabiliwa na mashitaka hayo adai amekamatwa kwasababu ya kudai Katiba.
Rais Samia amesema hayo hii leo katika mahojiano maalumu na chombo cha habari cha BBC na kueleza kuwa kwakuwa suala hilo lipo mahakamani hivyo hawezi kulizungumzia kiundani na kuichia mahakama iidhihirishie ulimwengu kama shutuma dhidi ya Mbowe ni za kweli ama la.
“Lakini kama utakumbuka Mbowe kipindi kirefu hakuwepo nchini alikuwa Nairobi sasa kwanini kakimbia sijui lakini alipoingia tu nchini kaitisha maandamano ya katiba na madai ya katiba,Nadhani ni calculation akijua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hivyo lugha ambayo anaitumia akikamatwa aseme kwasababu ya katiba kwasababu tumeitisha katiba”amesema Rais Samia.

Freeman Mbowe akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi na mashitaka ya ugaidi yanayomkabili.
Aidha ameongeza uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ulianza mwaka jana na baada ya polisi kukamilisha upelelezi wao dhidi yake ndipo walipoamua kuendelea na kesi huku akisisitiza mashitaka hayo dhidi ya Mbowe hayajachochewa na sababu za kisiasa.
“Ninavyojua mbowe alifunguliwa kesi mwezi wa tisa mwaka jana , kwahiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashitaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi nadhani wenzie kesi zao zimesikilizwa wenggine wamepewa hukumu zao wanatumikia.Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujaisha uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda tumeingia kwenye uchaguzi amemaliza uchaguzi lakini sasa hivi polisi wamekamilisha uchunguzi wao wamemuhitaji waendelee na kazi yao”amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia amesema Vyombo vya habari nchini Tanzania vina uhuru wa kutosha na mpaka sasa hakuna chombpo chochote cha habari kilicholalamika na vyombo vyote vinavyofuata sheria na maadili ya kazi zao vinafanya kazi.
“wana uhuru wa kutosha, na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine kwa sababu viongozi inabidi mvae ngozi ngumu mwangalie lakini wakati mwingine kusema kwao bora umpe mtu nafasi kuawasilisha alichonacho, atoe umsikie kama Kiongozi useme aaah kumbe kuna kulalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko kuwabana hawasemi kujua wanafukutwa na nini ndani” Rais Samia.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA