February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA GHANA, KUPOKEA TUZO

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesafiri kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya ziara ya kikazi, ikiwemo kupokea tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye, ya mafanikio ya Serikali yake katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu.
“Rais Samia anaondoka nchini leo kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo. Anatyarajia kupokea tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa wakuu wa nchi iliyofanya vizuri zaidi,” imeeleza taarifa ya Haniu.
Taarifa ya Haniu imesema, Rais Samia anatarajiwa kushikiri mdahalo wa wakuu wa nchi utakaojadili fursa zilizomo na changamoto zinazozikabili nchi za Afrika ikiwa pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, kupanda kwa bei ya vyakula na matumizi ya nishati endelevu.