March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS SAMIA ASISITIZA MSAADA WA KISHERIA KWA WANYONGE.

Samia Suluhu Hassan-Rais wa Tanzania.

Na: Anthony Rwekaza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesisitiza suala la kuzingatia utu pale wananchi wasio jua taratibu za kisheria wanapopeleka kesi Mahakamani kuwa Serikali inatakiwa kuwapatia Mawakili wale ambao hawana uwezo huo.

Akizungumza leo Februari 2, 2022 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria Nchini kwenye ukumbi Chinangali Park uliopo Jijini Dodoma, ambapo alikuwa mgeni rasmi, amesema utu unatakiwa kuzingatiwa, ambapo amedai kuna wananchi ambao wanapeleka kesi Mahakamani lakini hawajui njia za kupitia, amedai wenye uwezo utegemea mawakili lakini kwa wasio na uwezo amesema Serikali wana jukumu la kumpatia Wakili.

“Utu uzingatiwe katika utoaji wa Haki
Na hapo masharti ya kiufundi nina maana gani? Kwamba Mwananchi anapoleta kesi yake mahakamani, hajui chochote, hajui apite njia gani. Anategemea Wakili kwa mwenye uwezo wa kuweka Wakili na asiye na uwezo Serikali tuna jukumu la kumpatia Wakili lakini sidhani kama wote wanapata mawakili.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Kufuatia hali hiyo Rais Samia Suluhu Hassan amesema upo uwezekano amesema upo uwezekano wa anayeweza kuwa amedhulumu akawa na uwezo wa kuweka Wakili, ambapo amedai mawakili hao wanaweza kutumia jia za kiufundi jinsi ya kukwepa vipengele jambo ambalo linaweza kumyima haki anayestaili. Lakini amesema pamoja na kutumia sheria kiufundi Mahakamani, kwa wanahusika na kutoa haki kuzisikiliza nafsi zao wakati wa uamuzi ili kufahamu kama wanatenda haki.

“Anayedhulumu, anayeshitakiwa ana uwezo wa kuweka wakili. Kwahiyo mawakili hawa hutumia njia zao za kiufundi jinsi ya kukwepa vipengele na kuweza kumtia hatiani, au kumnyima haki mwenye haki, kwahiyo, niseme tu kwamba Mahakama pamoja na kutumia vifungu vya sheria kiufundi mahakamani, kubwa kwa wewe unayetoa haki ni kuisikiliza nafsi yako, je, hapa natenda haki au sitendi haki?” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Pia Rais Samia Suluhu Hassan amesema maboresho ya teknolojia katika Mahakama
yameonesha nia thabiti na ya dhati kuonesha kuwa Tanzania na wadau wote wa Haki sasa, hususani wale wanaopata changamoto kuweza kuzifikia huduma za Haki mahakamani na kuzipata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Aidha Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma amesema wadau wengi wanaohusika na myororo wa Mahakama utumia tehama ambazo haziwasiliani kwa faida ya utoaji haki, amesema atua inayotakiwa kufuata ni kuifanya mifumo hiyo iongee kwa faida ya kutoa huduma na sio kutumia tu tehama kwa lengo la kukusanya madhuhuri.

Ukiangalia wadau wengi wa myororo wa haki wengi wanatumia tehama, lakini ile mifumo haiongei, haiwasiliani kwa faida ya utoaji wa haki, kwahiyo hatua inayofuata ni ile ni ile mifumo yetu iongee kwa faida ya kutoa huduma, tusitumie tu tehama kwa faida kukusanya madhuhuri lakini tuhakikishe tunatumia mifumo hiyo Ili kuhakikisha tunatoa haki kwa wananchi” amesema Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma

Vilevile Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Prof. Edward Hosea, amesema mwananchi hana budi kupata ushauri wa mawakili ili anapoamua kufanya uamuzi wa jambo lolote mfano kuingia mikataba ya biashara ili ajue anafanya nini, na pale mikataba hiyo inapovunjika ajue hatua za kuchukua.

“Mwananchi hana budi kupata ushauri kutoka kwa mawakili ili anapoamua kufanya jambo fulani kwa Mfano, kuingia mkataba wa biashara awe ameelewa athari nini afanye katika mkataba huo unapovunjika” amesema Rais wa TLS, Prof. Edward Hosea

Lakini pia Prof. Hosea amependekeza kuunganisha kada za mawakili, baina ya kada ya mawakili wa Serikali na kada binafsi, pia ameshauri kuundwa chama kimoja cha mawakili wote, huku akishauri Serikali kabla ya kuwatafuta wataalamu wa sheria kutoka nje iwatumie TLS ili kukuza vipaji vya ndani na kupunguza gharama.

Maadhimisho hayo ambayo ufanyika kila mwaka, kwa Mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo “1Zama za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Safari ya Maboresho Kuelekea Mahakama Mtandao”, maadhimisho hayo uambatana na majukumu tofauti ikiwemo kutoa msaada wa kisheria, kutoa elimu ya kisheria kwa Wananchi pamojo na kuweka mikakati mbalimbali katika kada ya sheria.