February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS MWINYI;SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi,Dkt Hussein Mwinyi amesema serikali inatambua na kuthamini mchango wa Asasi za kiraia katika kuleta maendeleo ya taifa.

Rais Dkt Mwinyi amezungumza hayo mapema hii leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Zanzibar ulioanza hii leo na utahitimishwa rasmi Machi 14,2022.Mkutano huo unaofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip na kuwakutanisha na kuyaleta pamoja na kukutanisha mashirika zaidi ya 200 kutoka Tanzania Bara naZanzibar,wadau mbalimbali,sekta binafsi,

“Nilihimiza sana juu ya umuhimu wa kushirikiana baina ya serikali,sekta binafsi na makundi yote ndani ya jamii katika ujenzi wa nchi yetu,”amesema Rais Mwinyi akisisitiza kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitahakikisha AZAKI zilizoanzishwa zinatimiza malengo na matarajio ya kuanzishwa kwake.

Aidha ameongeza kuwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa AZAKI Zanzibar watapata fursa ya kujadili namna gani wataweza kukuza na kuboresha mashirikiano baina ya AZAKI na serikali na kujadiliana kuhusu namna bora ya uendeshaji wa usimamizi wa Asasi za Kiraia.

Rais Dkt  Mwinyi amesema anafahamu kuwepo kwa changamoto nyingi za utendaji na uendeshaji zinazoikumba sekta ya Azaki na kuwataka wanaAzaki kutokubaliana na malengo mema ya kuanzishwa kwa taasisi hizo yanatiwa dosari na wanaoanzisha taasisi hizo wakiwa na malengo na ajenda za siri.

“Hakikisheni kila taasisi inayoanzishwa inatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia malengo yaliyobainishwa wakati wa usajili na kwakuzingatia sheria za nchi yetu,”

Aidha amesema Azaki zina wajibu wa kuhakikisha mapambano dhidi ya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma yaliyoanzishwa yanajumuishwa katika Asasi za kiraia.

“Ni matumaini yangu suala la vita dhidi ya rushwa na utawala bora nalo mtalijadili katika mkutano huu,” amesema Rais Mwinyi.

Kwa upande mwingine Rais wa Zanzibar,Dkt Hussein Mwinyi amezitaka Azaki kuwa wabunifu ili kuepuka changamoto za upatikanaji wa fedha za kuendeshea taasisi hizo.

“Kuweni wepesi kwa kuandika maandiko ya miradi katika maeneo muhimu ya maendeleo yetu ambayo wahisani katika nchi mbalimbali wako tayari kuyachangia,”amesema Rais Dkt Hussein Mwinyi akitumia fursa hiyo kuwahimiza wahisani wa nje kuendelea kushirikiana na kufany kazi kwa karibu na Azaki ili ziendelee kutoa huduma kwa wananchi na kuchangia katika maendeleo.

Pia ametoa wito kwa ofisi ya Mrajis wa Azaki,Zanzibar kuendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi zote ambazo zimesajiliwa ili iweze kufahamu hali halisi ya maendeleo ya asasi hizo pamoja nakazi wanazozifanya.

“Pamoja na kutekeleza kazi mnazozifanya AZAKI zina wajibu mkubwa wa kuhakikisha tunaendelea kuishi kwa amani na utulivu,nina furaha kupata taarifa kuwa taasisi ya FCS na mashirika mengine ya kimataifa yanatoa ufadhili wa asasi za kiraia ili ziweze kutekeleza mradi wadumisha amani Zanzibar,”amesema Rais Dkt Mwinyi.

Katika Mkutano huo ambao umeandaliwa na Jumuiya ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Zanzibar (ANGOZA),PACSO na Kamati ya Maandalizi ya AZAKI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum Zanzibar unalenga kuimarisha mashirikiano baina ya Serikali na qAsasi za Kiraia visiwani Zanzibar ambapo washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuonyesha kazi zinazofanywa na Asasi za Kiraia katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Pia kupitia Mkutano Mkuu wa AZAKI Zanzibar,2022 itasaidia katika kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu kazi zinazofanywa na AZAKI,kuhamasisha uwazi na uwajibikaji,Kuongeza uelewa kuhusu sheria zinazoongoza Asasi za Kiraia na pia wadau watapata fursa ya kuweza kujadili mikakati mbalimbali juu ya namna ambavyo AZAI zinaweza kufanya kazi zinazoweza kuleta maendeleo nchini.

Mbali na maonesho ya kazi za AZAKI ,Mkutano huu Mkuu utafuatiwa na semina mbali mbali zinazolenga kuziongezea uwezo Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa mipango na shughuli za Taasisi hizo pamoja na kuona mchango wao katika ujenzi wa Taifa,na kuangalia changamoto zinazokabili sekta ya AZAKI na kujadiliana kuhusu namna bora ya kutatua changamoto hizo.

Aidha katika Mkutano huo Mkuu wa AZAKI Zanzibar,unatarajiwa kuwakutanisha na kuyaleta pamoja na kukutanisha mashirika zaidi ya 200 kutoka Tanzania Bara naZanzibar,wadau mbalimbali,sekta binafsi, Wizara na vyombo vya habari ambapo watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuonyesha kazi zinazofanywa na Asasi za Kiraia katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha rasmi Mkutano Mkuu wa Asasi za Kiraia Zanzibar mnamo tarehe 14,2022.