Na Loveness Muhagazi
Katika Kongamano Hilo Rais Mwinyi anatarajia kujadiliana na Watetezi wa Haki za Binadamu visiwani Zanzibar juu ya changamoto zinazomkumba mtoto wa kike Pamoja na namna ya kutokomeza vitendo vya Udhalilishaji sambamba na kuzindua mfumo, huku taasisi ya ZAFELA Ikitoa Tuzo kwa wafadhili.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi hii Leo amehudhuria Kongamano la kutokomeza vitendo vya Udhalilishaji lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) ambalo ni Shirika Mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC kutoka visiwani Zanzibar.
Kongamano Hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdul Wakil Visiwani Zanzibar linatatajiwa kuhudhuriwa na wageni wengine wa mamlaka mbali mbali wakiwemo Jaji mkuu wa Mahakama ya Zanzibar, Makamishina wa Polisi, Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka (DOO), Mrajis wa Mahakama ya Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na watoto, wakurugenzi wa Asasi mbali za Kiraia na Taasisi mbali mbali ziliwemo FCS, LSF, KAS na THRDC na wawakilishi mbali mbali kutoka mashirika Watetezi wa Haki za Binadamu visiwani Zanzibar.
Habari Zaidi
KIKOSI KAZI KITASAIDIA KULETA MARIDHIANO – JK
NI MIAKA MITANO SASA TOKEA LISSU ASHAMBULIWE
SHAHIDI JAMHURI AELEZA KINA MBOWE WALIVYOSUKA MPANGO WA KUTENDA UGAIDI