February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS ALIYEKIMBIA NCHI YAKE AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA AKIWA UHAMISHONI

Rais wa Afghanstan aliyekimbia nchi yake siku ya Jumapili, Ashraf Ghan amezungumza kwa mara ya kwanza akiwa uhamishoni katika nchi ya Umoja wa nchi za Kiarabu (UAE) na kusema haogopi kufa kiheshima kwa kunyongwa ila hawezi kuona waafghan wakifedheheka, na kusema kwasasa yupo katika mazungumzo ili aweze kurejea tena nchini mwake.

“Nina ujumbe wa muhimu sana kwenu, sina nia ya kukimbia na kubakia uhamishoni, kwa sasa nipo UAE ili kusiwepo kwa umwagaji wa damu na kuona vurugu zinasitishwa,kwa sasa nipo katika mazungumzo ili niweze kurejea tena Afghanstan na ninachukua jitihada zote kulinda haki,kuhifadhi maadili yetu na uislam wa kweli pamoja na mafanikio ya Taifa letu la Afghanstan,”amesema Ghani  

“Kama ningebakia huenda ningenyongwa mbele ya umati wa waafghan na aibu ile ingejirudia.Siogopi kufa kwa heshima na sitaogopa lakini sitaweza kuona fedheha kwa waafghan kwahiyo nililazimishwa kuondoka”

Aidha amewataka wananchi wa Afghanstan kutowaamini wale wanaowaambia kuwa amekimbia taifa hilo kwa maslahi yake mwenyewe.

“Msimwamini mtu yeyeote atakayewaambia kuwa Rais wenu nimeamua kuwauza na kukimbia nchi ili kuokoa maisha yangu peke yangu,Niliondoka Afghanstan kiasi kwamba sikuweza hata kubadili ndala katika miguu yangu na kuvaa viatu,”