February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

RAIS AJIUZULU,KISA KATIBA KUMNYIMA BAADHI YA MAMLAKA

Rais Armen Vardani Sarkissian wa Armenia.

Rais Armen Vardani Sarkissian wa Armenia,ametangaza kujiuzulu katika nafasi ya Urais,kwa kile alichodai kuwa,Katiba ya sasa ya nchi hiyo inainyima nguvu ofisi ya Rais kushawishi mambo muhimu,ikiwemo sera ya utatuzi pindi taifa linapoingia katika mizozo.

Barua ya kujiuzulu kwake,haijataja jambo moja kwa moja,lililomfanya kuchukua uamuzi wa kuachia Urais,na badala yake ametaja mambo kwa ujumishi.

“Rais anawezaje kukosa nguvu ya ushawishi katika michakato nyeti ya sera za nje na ndani ya nchi,katika nyakati ambazo nchi na watu wake wanapoingia katika matatizo?”amehoji Rais Sarkissian,katika waraka uliochapishwa kwenye tovuti ya Rais.

Mwaka 2021,Rais Sarkissian aliingia katika mgogoro mkubwa na Waziri wake Mkuu Nikol Pashinyan,baada ya kutofautiana kimsimamo,katika baadhi ya mambo,ikiwemo kuondoshwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,kufuatia vita kali iliyoibuka kati ya Vikosi vya Armenia na kundi lawapiganaji la Azerbaija,wakigombea eneo muhimu la Nagorno-Karabakh,hali iliyosababisha watu kuandamana katika majengo na ofisi mbalimbali za Serikali nchini humo.

Marekebisho ya Katiba ya Armenia ya mwaka 2015,yaliifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri kamili,inayotegemea Bunge kufanya maamuzi,huku Mamlaka na nguvu za kiutawala,zikiwa kwa Waziri Mkuu,na siyo Rais.

Rais Sarkissian,aliingia Madarakani mwaka 2018 akitokea kuhudumu kama Balozi wa kudumu wa armenia nchini Uingereza,tangu mwaka 1998,na amekuwa Waziri Mkuu wa Armenia kati ya mwaka 1996-97