Na Antony Rwekaza
Kamanda Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amethibitisha kutokea vifo vya Watu saba kufariki dunia kutokana kupigwa na radi katika maeneo tofauti kwenye Wilaya za Nkasi na Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akieleza tukio hilo Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nkandasi, Given Kisantola amesema tukio la kwanza lilitokea Februari 26 saa 9 alasiri kwenye Kijiji cha Nkandasi wilayani Nkasi, ambapo Watu watano amabao walikuwa wakifanya kibarua cha kupanda maharage shambani walikufa papo hapo huku 14 kati yao walijeruhiwa baada ya kupigwa radi wakiwa wamejikinga kwenye nyumba kwenye shamba hilo.
Ameeleza kuwa watu hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao, baada ya kuona mvua imeanza kunyesha waliacha kupanda maharage na kuamua kukimbilia kwenye nyumba hiyo ili kujikinga na mvua.
Aidha, tukio lingine tukio jingine lililotokea siku hiyo ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijajulikana(jina lake rasmi lilikuwa halijatabulika) mkazi wa kijiji cha Luwa Manispaa ya Sumbawanga, amekufa papo hapo yeye na mtoto wake baada ya kupigwa radi wakiwa shambani wanalima.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA