February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PROF. NGOWI AFARIKI DUNIA AJALINI

Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Honest Ngowi, amefariki dunia kwa ajali , baada ya gari lake kuangukiwa na kontena akiwa safarini kuelekea Morogoro, akitokea Dar es Salaam. Prof. Ngowi amefariki dunia maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.

“Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari, wakiwa njiani kuelekea kampasi kuu. Taarifa kamili zitawajia hivi punde,” imesema taarufa ya Mzumbe.

Enzi za uhai wake, Prof. Ngowi alikuwa mchambuzi wa masuala ya uchumi na mtafiti.