February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

POLISI :TUNAFANYA UCHUNGUZI TUKIO LA MCHIMBAJI MADINI KUPIGWA RIASI, WASISITIZA UTULIVU

Na: Anthony Rwekaza

Kufatia madai ya mauaji ya mtu mmoja ambaye ni Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Mwamala, Kijiji cha Igumanghobo, Kata ya Idukilo Mkoani Shinyanga aliyekuwa akichimba madini katika Kijiji cha Mwang’holo, Kata ya Mwadui Lohumbo, kudaiwa kuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi wanaolinda eneo la Mwekezaji Kampuni ya El-Hillal Minerals Ltd, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, amekili kupokea madai hayo.

Akizungumza na chombo cha habari cha kuaminika Nchini Tanzania Kamanda huyo amesema tukio hilo lina muda tokea lilipotiwe hivyo kulizungumzia zaidi linaweza kuonekana tukio jipya kwa umma, lakini amedai kuwa uchunguzi wa madai hayo unaendelea hivyo ukikamilika watachua atua zaidi za kisheria”

“Hilo ni tukio ni la muda nikilizungumza leo itaonekana kama ni jipya. Lakin Uchunguzi unaendelea, ukikamilika hatua zitachukuliwa.” Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga

Pia alipoulizwa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa kwa mtuhumiwa na kama bado anaendelea na majukumu yake kama kawaida amesema kuwa hawajamkamata na anaendelea na majukumu yake kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika na amesita kutaja jina lake kwa madai ya sababu za kiuchunguzi.

“Hatujamkamata, anaendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa uchunguzi haujakamilika, wala siwezi kumtaja jina kwa kuwa tutaharibu uchunguzi.” Amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,

Amesisitiza kuwa amekuwa akiwataka wananchi kuwa watulivu na amewataka endapo linatokea tatizo kwao wasijichulie hatua mkononi, amedai kuna wakati askari anaweza chukua hatua tofauti kwa lengo la kujihami.

“Nimeshazungumza na ninarudia wananchi wawe watulivu na kama kunakuwa na tatizo lolote wasichukue hatua mkononi, maana askari anaweza kufanya hivyo katika njia ya kujihami” amesema Kamanda wa Polisi Mkoa Shinyanga,

Amewataka Wananchi kutovamia askari kwa kuwa kama kuna malalamiko yao kwa wawekezaji au ardhi, isipokuwa amewataka kuzingatia taratibu za kisheria, ambazo amezitaja kama vile kwenda mahakamani na kwenye vyombo vingine vya kufikisha kile wanachokilalamikia na siyo kujichukulia hatua mkononi jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Itakumbukuwa Marehemu ametajwa kwa jina la Cosmas Hamis Kusililwa umri wa miaka 25 ambaye amekuwa akijihusisha na uchimbaji mdogo inadaiwa alipigwa risasi Machi 10, 2022 akiwa nje ya eneo la mwekezaji huyo ambako wachimbaji wengi wadogo ujishughulisha na uchimbaji wa Madini ya Almasi kwa lengo la kujipatia kipato.

Aidha mara baada ya taarifa hizo kuenea, Tukio hilo limelaaniwa vikali na viongozi mbalimbali kikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan asitishe uwekezaji wa mwekezaji huyo ambaye anadaiwa kushindwa kuliendeleza eneo alilopewa kwa zaidi ya miaka 15 hivi sasa.

Vilevile kwa upande wao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, William Jijimya na Katibu wa CCM Wilayani humo, Peter Mashenji wamesema kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na kwamba wakazi wa Kishapu, ameongeza kuwa wakazi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo hawahitaji mwekezaji anayewafanyia vitendo vya ukatili wananchi, lakini pia amemuomba Waziri wa Madini kuchukua hatua haraka kufuatia madai hayo.