March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PINGAMIZI UPANDE WA MBOWE NA WENZAKE LATUPWA, KIELELEZO KUPOKELEWA

Na Antony Rwekaza

Mahakama imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na upande wa utetezi wanaomtetea Freeman Mbowe na wenzake, lililotaka mahakama kutoipokea nyaraka ya hati ya uchukuaji mali iliyotolewa na shahidi wa nane wa Jamhuri ASP, Jumanne Malangahe, wakidai nyaraka hiyo ina makosa ya kisheria kufuatia kunukuu mabadiliko ya sheria ambayo hayapo.

Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo akitoa uamuzi huo leo Novemba 9, 2021 Mahakamani, amesema anaungana na upande wa utetezi kuwa kuna ukweli wa nyaraka hiyo kunukuu kimakosa mabadiliko ya sheria ambayo hayapo, lakini amesema tatizo hilo linatibika kwa mujibu sheria, akirejea baadhi ya zilizoamuliwa kwenye Mahakama ya Rufani, amesema taratibu za kisheria zinatoa nafasi ya kupima uzito wa hoja kwa upande wa washtakiwa endapo zinaeleza wanavyoweza kuathiriwa na nyaraka hiyo ambayo ina mapunfu ya kisheria katika kunukuu.

Hivyo Jaji amesema hoja za upande wa utetezi hazionyeshi uzito wa kuathiriwa na uamuzi wa nyaraka hiyo ikipokelewa Mahakamani, hivyo Mahakama imetambua kupokea nyaraka hiyo kuwa kielelezo, na kutupilia mbali hoja za upande wa utetezi.