February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PINGAMIZI LA MBOWE NA WENZAKE LAKATALIWA, MAHAKAMA YAKUBALI KUPOKEA KIELELEZO

Na Antony Rwekaza

Mahakama imetoa uamuzi wa kukubali ombi la upande wa Jamhuri, kupokea barua ya kielelezo cha shahidi namba mbili H4323 DC Msemwa, ikiwa ni kufuatia upande Mawakili wa utetezi kwenye Kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi namba 16/2021 kuweka pingamizi la kupinga kielelezo hicho kupokelewa Mahakamani.

Ambapo walidai akikujengewa msingi mzuri na kuwa kilijielekeza kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Dodoma, wakitoa hoja kuwa ni kinyume na taratibu ikiwa kwenye ushahidi haionyeshi kuwa shahidi ni muajiriwa kwenye ofisi hiyo, lakini kwenye uamuzi uliotolewa na Jaji Joachim Tiganga anayesikilza kesi hiyo emesema kielelezo hicho licha kutoka kwenye ufisi ya Taifa ya Mashtaka lakini kilitolewa na kupokelewa na mtu sahihi hivyo kinajitosheleza.

Jaji Tiganga amesema kielelezo kingeibua mashaka kama endapo kingechelewa kumfikia mlengwa ambaye ni shahidi kwa kupitia kwenye mikono mbalimbali, lakini kilipelekwa kwa shahidi ambaye Mahakama imemtambua kuwa ni ‘competent’, hivyo ameruhusu kielelezo hicho kisomwe Mahakamani kabla ya kupokelewa.

Lakini upande wa utetezi kabla ya Shahidi kuanza kusoma wameikumbusha Mahakama juu ya tukio lilotokea Ijumaa Novemba 12, 2021 kwa shahidi kukutwa na diary pamoja na simu akiwa kizimbani, Mahakama imekubali wawasilishe hoja zao kuhusu namna wanavyoweza kuathiriwa na tukio hilo, wamedai ni kinyume na sheria na taratibu hivyo wameitaka Mahakama kutoutambua ushahidi wa shahidi huyo, wamedai ili shahidi kuwa na kitu chochote kizimbani tofauti na anavyokuwanavyo wakati wa kiapo, anatakiwa kupewa idhini na Mahakama.

Ikumbukwe Kesi hiyo inamkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu wakiwemo wanaodaiwa walikuwa makomadoo wa Jeshi, wakikabiliwa na mashtaka ya Ugaidi tofauti ikiwemo kutuhumiwa kula njama za kulipua vituo vya mafuta, kuwadhuru viongozi wa Serikali kufunga barabara, ikidaiwa kuwa lengo Nchi hisitawalike kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.

Ndani ya kesi ya msingi, kesi ndogo ilibuka kufuatia Mawakili wa upande wa utetezi kuweka pingamizi kuhusu kuhusu Mahakama kutopokea na kuyatambua maelezo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa namba tatu Mohamed Ling’wenya, ambapo kati ya hoja zao kwenye kesi hiyo ndogo wanadai yalichukuliwa baada ya mshitakiwa huyo kulazimishwa na kwa vitisho.