February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PAPA FRANCIS ASHINIKIZWA KUINGILIA MZOZO WA GAZA.

Na Leonard Mapuli

Watu Zaidi ya 200 wakiwemo Watoto 58 wameripotiwa kupoteza Maisha eneo la Gaza kufuatia mashambulio ya anga yanayoendelea kufanywa na Israel kwa nchi ya Palestina.

Mzozo huo ambao umekuwepo dahari na dahari umeingia juma la pili baada ya Israel kuanzisha tena mashambulizi baada ya Waziri wake mkuu Benjamin Netanyahu kusema kuwa mashambulizi si ya kukoma leo wala kesho.

Milipuko imelichakaza jiji la Gaza leo Jumatatu Mei17  kutokea Kaskazini Kuelekea kusini mwa jiji hilo ambapo kumefanywa mashambulizi ya makombora mazito  ya masafa marefu yaliyodumu kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa yale ya jana (Jumapili) yaliyoua Wapalestina 42,na kujeruhi Mamia wengine.

Kikundi cha Hamas kinachoukalia mji wa Gaza kimeshambulia pia kwa roketi majiji ya Ashkelon na Beersheba ya nchini Israel na kuua watu 10 wakiwemo Watoto wawili.

Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa lililoketi hapo jana (Jumapili Mei 16) lilishindwa kufikia muafaka wa Pamoja juu ya mzozo huo huku China ikimshutumu Marekani kukwamisha baraza hilo kuwa na kauli moja.

Rais Reccep tayyiping Erdogan wa Uturuki amemuomba kiongozi wa kanisa Katoliki dunia Papa Francis kuingilia kati mzozo huo huku  Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu yakiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuchunguza masuala kadhaa ikiwemo kushambuliwa kwa majengo ya vyombo vya Habari.

Inakadiliwa wastani wa Watoto watatu wanajeruhiwa ndani ya saa moja tangu kuanzishwa kwa mzozo huo Mei 10,hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea Haki za Watoto la Save the Children.Baadhi ya miundombinu ikiwemo ya Umeme na mawasiliano imeharibiwa sana katika eneo la ukanda wa gaza.