February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PAPA FRANCIS AENDELEA KULAZWA HOSPITALINI GEMELLI

Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameendele kulazwa  katika Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma kwa ajili ya kufanyia upasuaji  mkubwa kwenye utumbo mpana itakayofanywa na Profesa Sergio Alfieri na Baada ya upasuaji huo, Hospitali ya Gemelli itatoa taarifa kuhusu hali ya mwenendo wa afya ya kiongozi huyo.

Msemaji mkuu wa Vatican Dkt. Matteo Bruni amesema papa Francisko, amelazwa kwenye Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma siku ya Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji  mkubwa kwenye utumbo mpana Katika Hospitali hiyo ya Gemelli .

Kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji huo mkubwa,Jumapili  Papa Francis alisali na kutafakari na waamini pamoja na mahujaji waliofika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuhusu “Kashfa ya Fumbo la Umwilisho”.

Waamini wa dhehebu hilo wameendeleo kumuombea kiongozi wao huyo ili arejee katika hali yake ya kawaida

.