December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

PADRI ALIYEWABUSU WANAFUNZI AFUKUZWA

Kanisa la Anglikana nchini Ghana  limemfukuza padre Balthazar Obeng Larbi wa chuo cha Mt.Monica aliyeonekana katika video iliyosambaa mtandaoni akiwabusu wanafunzi watatu wa kike, Kanisa hilo limefikia uamuzi huo siku ya Jumannne baada ya kukaa kikao na kujadili suala hilo.

Padre Balthazar Obeng Larbi amezuiwa kufanya shughuli zote za utumishi wakati uchunguzi ukiwa unaendelea na kufuata ushauri kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili kushughulia suala la padre huyo.Katika taarifa ya kanisa hilo, imeelezea kusikitishwa na tukio hilo na uchunguzi umeanza mapema.

Taarifa hiyo  imeeleza kuwa  wanafunzi hao watatu watapewa ushauri nasaha ili kuondoa mshtuko waliopata.Katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha kiongozi wa dini aliyevaa nguo za kijani akiwaita wanafunzi watatu wa kike kwenye mimbari, na kisha akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu, huku kelele za kushangiliwa zikisikika.